Breaking News

RAIS KAGAME AMALIZA ZIARA YAKE YA JIJINI DAR ES SALAAM NA KUREJEA NCHINI RWANDA.


Rais wa Tanzania John Magufuli akisalimiana na  mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Teminal 1 wakati akijiandaa kurejea nchini Rwanda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili jijini Dar es Salaam.


Rais wa Tanzania John Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Paul Kagame  wakipita kwenye Gadi ya heshma iliyoandaliwa na  Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Tanzania John Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati akimsindikiza kwenda kupanda ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania John Magufuli akiagana na mgeni wake Rais Paul Kagame katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Tanzania John Magufuli akizungumza na vikundi mbalimbali vya ushehereshaji katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumsindikiza mgeni  wake Rais Paul Kagame.

Rais wa Tanzania John Magufuli akiagana na vikundi mbalimbali vya ushehereshaji  kwa kuwapungia mkono mara baada ya kumsindikiza mgeni  wake Rais wa Rwanda Paul Kagame. PICHA NA IKULU

No comments