Breaking News

RAIS MAGUFULI AWAMWAGIA SIFA WANAWAKE.


Rai wa Tanzania, John PombeMagufuli,amewasifia wanawake kwa kusema wanafanya kazi kubwa kwaajili ya Tanzania hivyo amewataka wazidi kudumisha upendo na mshikamano kwa maslahi yao pamoja na nchi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Machi8, 2019, Jijini Dar es salaam Mara baada ya  kuagana na mgeni wake Rais wa Rwanda, Paul Kagame leo aliyekuwa nchini kwa Ziara ya Kikazi. 

Rais Magufuli amesalimiana na wananchi wa Dar es Salaam waliojitokeza kumuaga Rais Kagame ambao wengiwao walikuwa ni wanawake na kuwatakia heri ya Siku ya Wanawake ambayo huadhimishwa tarehe 08 Machi, kila mwaka duniani kote.

Katika salamu zake Rais Magufuli amewashukuru Wanawake wote hapa nchini kwa mchango wao mkubwa hapa nchini na kusisitiza kuwa Serikali inatambua juhudi hizo.

“Mungu awabariki sana akina Mama, mnafanya kazi nzuri kwaajili ya Taifahili, endeleeni kuimarisha umoja wa Watanzania wote, Serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri zinazofanywa na akina Mama, endeleeni kutembea kifua mbele, Mungu atawalinda" amesema Magufuli na kuongeza kuwa 

"Na mimi sasa hivi naondoka kwenda kumuona Mama yangu hospitalini katika siku yake hii, pia natoa shukrani nyingi kwenu na kwaviongozi wa Mkoa na Wilaya kwa jinsi mnavyojitolea kuwapokea na kuwaaga vizuri wageni wetu” amesisitiza Rais Magufuli.

No comments