Breaking News

SIMBA ITACHUKUWA UBINGWA AFRIKA KAMA, WATAAMINI NA KUFANYIA KAZI MANENO HAYA YA WAZEE.

"YALIYOPITA SI NDWELE, TUGANGE YAJAYO"
Klabu bingwa Afrika ni Mashindano makubwa na ya muda mrefu ambayo yalianza mwaka 1965, yakiitwa hivyo na kuendeshwa kwa mtindo wa mtoano kuanzia raundi ya kwanza mpaka fainali.

1997 Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF ilibadilisha mtindo wa uendeshwaji wa mashindano hayo kwa kuanzisha hatua ya Makundi, ndipo jina la mashindano hayo likabadilika toka Klabu bingwa mpaka Ligi ya mabingwa.

Kulikuwa na makundi mawili yenye kubeba timu nne kila moja, mfumo huo mpya ulizifuta hatua za robo na nusu fainali, hivyo vinara wa kila kundi walikwenda moja kwa moja fainali.

Mfumo huu ulileta tiligivyogo(haukueleweka kwa wengi), mfano mwaka 1998, Yanga ilipo fuzu hatua ya Makundi Katibu mkuu wa TFF wakati huo ikiitwa FAT, Ismail Aden Rage, alinukuliwa akisema kwamba Yanga wametinga hatua ya nusu fainali., yawezekana alikuwa hajaelewa vizuri mfumo huo.

2001 CAF wakairudisha hatua moja ya Nusu fainali iliyo futwa 1996, ambapo timu mbili za juu zilifuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali, na washindi kutinga fainali.

2017 CAF wakaongeza idadi ya timu za kufuzu hatua ya makundi kutoka 8 hadi 16 na kuongeza makundi kutoka mawili hadi manne, hapo ndipo hatua ya robo fainali iliporejea tena tangu kusitishwa kwake Mwaka 1996.

Magoli mawali ya Mohamed Hussein na Clatous Chama dhidi ya AS Vita, yametosha kuifikisha Simba hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania tangu mwaka 1994.

Hayo yameisha, yamepita, historia imesha andikwa upya, waswahili wanasema yaliyopita si ndwele, hivyo kwa sasa Wachezaji, Viongozi, benchi la Ufundi, Mashabiki na wote wenye mapenzi mema na Simba hampaswi kufurahia na kuongelea hayo yaliyo kwisha kupita, mnapaswa kutazama yajayo sababu hayo ndiyo yatawapa furaha zaidi.

Kwa hatua ya robo fainali ni hatua ya mechi mbili tuu, Nyumbani na Ugenini, na ile sheria ya faida ya uwanja wa nyumbani hutumika kuamua atokeo, nani aende nani abaki., kama Simba itaruhusu magoli mengi ugenini kama awali na kuutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa ushindi wa idadi ndogo ya magoli, huo ndio utakuwa mwisho wa ushiriki wao.

Hivyo basi kila mmoja atazame vyema yajayo katika nafasi yake., WACHEZAJI ni vyema wakarejea kutazama video walivyo cheza mechi zote za nyumbani na ugenini, wabaini makosa yao, na wafanyie marekebisho mapema iwezekanavyo.

VIONGOZI waendeleze ushirikiano kati yao na wapenzi wa timu yao, waepushe chuki na migogoro kwa mafanikio yao na timu yao. 

BENCHI LA UFUNDI ni wakati wa kujikita katika kuinoa timu kwa levo ya kupambana hatua ngumu katika ligi kubwa na ngumu zaidi Afrika, ongezeni au badilisheni mbinu hasa kwa michezo ya ugenini, Simba inahitaji kubadilisha uchezaji wake hasa katika mechi za ugenini.

MASHABIKI hamasa yenu imedhihirisha kuwa ni muhimu kwa mafanikio ya klabu yenu, kwa michezo inayokuja muifanye Serikali kuanza kufikiria kuupanua uwanja wa Taifa, na ikiwezekana mfanye hivyo katika kila mechi za timu yenu hasa za ligi kuu ili kuipatia mapato timu yenu na kuifanya iwe tishio zaidi Afrika na Duniani kwa Ujumla.

Kutinga hatua ya robo fainali ni jambo kubwa lakini si lakujivunia kupita kiasi, kwanini ujivunie kufika hatua fulani wakati wenzako wanajivunia kutwaa mataji mengi kwenye michuano unayo shiriki..? 

kakuna kinacho shindikana, kila kitu kinawezekana,  naamini Simba itachukuwa ubingwa wa Afrika kama tu,  itaachana na yaliyopita kwa kuganga zaiidi yanayo kuja.
  

No comments