Breaking News

UBUNIFU UNATAKIWA KWA TIMU ZA UENDESHAJI HUDAMA ZA AFYA NCHINI.


Kamati za huduma za afya Mkoa  (RHMT)  na Wilaya(CHMT) nchini zimetakiwa kuwa wabunifu katika kutekeleza shughulizake na kuhakikisha wanaboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi mkoa kwaujumla ili kuleta matokeo bora kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Afya, OfisiyaRais,  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (OR-TAMISEMI),  Dorothy Gwajima katika kikao  cha  Mrejesho wa Utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Dodoma  na Halmashauri ya Chamwino leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Reforms uliopo katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Kikao hiki nimwendelezo wa mkakati maalumu wa kuzifunda timu za uendeshaji huduma za afya mikoanawilayakwakuanzianamkoawa Dodoma ili, ziweze kufanya uwajibikaji wenye matokeo na kuwaridhisha watumiaji wa huduma za vituo vya tiba na pia,  kuwa mfano wa kuigwa na mikoa mingine” be the center of excellence”.

Gwajima amesema kuwa,  ubunifu unaotakiwa ni kujenga mahusiano mazuri baina ya mteja na mtoa huduma za afya ili, mteja aweze kuwahuru na kujisikia faraja katika kupata huduma kuto ka kituoni hapo.

Vilevile,  amesema ni muhimu sana kuweka mkazo katika eneo la kitabibu na kuhakikisha kuwa,  huduma hizo ni sahihi,  salama na rafiki kwa vigezo vyote na wateja wanaridhika nazo.

“Mahusiano mazuri yanajengwa na ukarimu,  lugha nzuri kwa mteja na umahiri wa utendajikazi wenu wakitaaluma kwa ujumla wakati wa kuwahudumia wateja wenu. Wateja walio hudumiwa vizuri ndiyo ambao wanakuwa mawakili wazuri katika jamii yao kulingana na  jinsi ambavyo wao wamefurahia huduma zenu” Amesema Gwajima.

Lakini pia  Gwajima amewataka watoa huduma za afya kuwa na mpango kazi utakao weza kuwaongoza vyema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuweza kupimwa juu ya uwajibikaji wao pasipo shaka.

Gwajima ameeleza kuwa mpango kazi kwa mtumishi utasaidia kuweza kupata tathimini ya utekelezaji wa majukumu ya mtoa huduma za afya na kujua matokeo yapi yamefikiwa, kubaini changamoto zilizo jitokeza na kuzitafutia suluhisho ili kufikia malengo ya mtoa huduma aliyojiwekea katika mpango kazi  wake.

“Ili kupata tathimini ya utendaji kazi wawatoa huduma za afya amesisitiza kuhakikisha kila mmoja kuwa na taarifa ya uwajibikaji wake  huku ukiwa na takwimu sahihi  wakati wote. Ameongezea Gwajima.

Aidha  Gwajima amehitimisha kwa kuwataka watoa huduma za afya kutekeleza mipango kazi yao kwavitendo ili kuweza kupata matokeo chanya yatakayo onyesha mabadiliko katika sekta ya afya badala ya kuwa na watumishi ambao,  ukimuuliza niniamefanya siku hiyo anakuwa hana maelezo yenye takwimu bayana.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Samwel Seseja amesema atasimamia vyema maelekezo yalotolewa na Gwajima ili kuhakikisha utendaji kazi na uboreshaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi mkoa zinaboreka na kuimarishwa vizuri kwafaida ya watanzania.

No comments