Breaking News

LOWASSA AREJEA CCM NA KUPOKEWA NA RAIS MAGUFULI.


Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akiwasili katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kabla ya kutangaza rasmi kurejea katika Chama cha Mapinduzi CCM leo tarehe 1 Machi 2019.


Lowassa akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais John Magufuli akishuhudia. Wakwanza kushoto ni Kada wa CCM Rostam Azizi


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais John  Magufuli akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye ametangaza kurejea chama cha Mapinduzi CCM akitokea chama cha CHADEMA katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM Lumumba jijini Dar es Salaam


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Magufuli akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally wakizungumza jambo na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kurejea CCM akitokea CHADEMA.


Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisalimiana kwa furaha na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Magufuli akishuhudia.


Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akitangaza rasmi kurejea chama cha Mapinduzi CCM mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula, Katibu wa CCM Bashiru Ally, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamojan na Kada wa CCM Rostam Azizi.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Magufuli akizungumza kumkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye amerejea rasmi CCM.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  CCM Rais Magufuli akifurahia jambo  katika mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, Kada wa CCM Rostam Azizi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally. PICHA NA IKULU
No comments