Breaking News

DKT MPANGO ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA FEDHA MAREKANI.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip  Mpango (kushoto) akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinwumi Adesina, Mjini Washington DC, Marekani, kabla ya mkutano wa magavana wa Benki hiyo ambao ni Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54 zenye hisa kwenye benki uliofanyika katika ukumbi wa Willard Continental kujadili namna ya benki hiyo kuongezewa mtaji ili iweze kutoa mikopo kwenye nchi hizo kwa ufanisi zaidi

Dkt. Mpango  akifuatilia kwa makini mjadala wa namna Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB inavyoweza kuongezewa mtaji, Mjini Washington DC, Marekani, ambapo Tanzania imeridhia hatua hiyo.

Dkt. Mpango (kulia) akifuatilia kwa makini mjadala wa namna Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, inavyoweza kuongezewa mtaji, Mjini Washington DC, Marekani, ambapo Tanzania imeridhia hatua hiyo
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Washington DC

No comments