Breaking News

HAZARD AZICHONGANISHA LIVER POOL, DORTMUND.

Mshambuliaji tishio wa Borussia Monchengladbach Thorgan Hazard, ameonyesha nia ya kutaka kuondoka ndani ya miamba hiyo na kwenda kutafuta changamoto katika timu nyingine kwa msimu ujao wa 2019/20.

Borussia Monchengladbach,wangependa kumuuza Thorgan Hazard kwa klabu nje ya Bundesliga , kwa mujibu wa taarifa kutoka Het Nieuwsblad.

Sambaba na hilo Mbeligiji huyo mwenye miaka 26, amewaarifu Borussia Dortmund anataka kujiunga nao mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa taarifa kutoka Kicker.

Dortmund wanajiandaa kuwalipa Borussia Monchengladbach kiasi cha Pauni Milioni 35 kwa winga huyo wa kimataifa wa Ubeligiji ambaye mkataba wake unafikia tamati mwaka 2020.

Lakini Vinara wa Ligi kuu ya Uingereza wapo tayari kutoa kiasi cha Pauni Milioni 40, tano zaidi ya ile ofa ya Dortmund ili kufanikiwa kumnasa mbeligiji huyo majira ya kiangazi.
Je, Hazard atatua wapiii....! Dortmund au Liver pool.? tusubiri tuone.

No comments