Breaking News

KITUO CHA AFYA MUNDEMU KUONDOA KERO KWA WAJAWAZITO.

Na EZEKIEL NASHON, BAHI.

IMEELEZWA kuwa kukamilika kwa kituo cha Afya cha Mundemu, kilichopo kata ya Mundemu, Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kutapunguza kero zilizokuwa zikiwakumba akina mama Wajawazito wanaohitaji huduma ya uzazi, ambao walikuwa wakiifuata katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa viti maalumu, anayewakilisha kundi la vijana, Mariam Ditopile, wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM mkoa wa Dodoma, waliofika katika kituo hicho ikiwa ni kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya hiyo.

Amesema kukamilika kwa kituo hicho  kutasaidia kuokoa  gharama, na maisha ya mama na mtoto waliokuwa wakifuata huduma hiyo katika hospital ya mkoa Dodoma lakini kwa sasa wataipata karibu.

“Kukamilika kwa kituo hiki sasa kutapunguza gharama kwa sababu mnajua mwanzo mlikuwa mkifuata huduma mjini lakini serikali imejenga kituo hiki huduma zitasogea hapa mwanzo tulikuwa tukipoteza akina mama na watoto kwa sababu ya umbali lakini tunaona sasa huduma hii itapatikana hapahapa” alisema Mariam.

Aidha amesema lengo la ziara hiyo ni kuangalia hali ya kisiasa katika tarafa hizo na hasa katika kipindi hiki tunaelekea katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani ni kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo.

Kwa upande wake mganga mkuu wa kituo hicho Antony Mhimbira akitoa taarifa kwa kamati, amesema kituo hicho kinapokea rufaa ya wagonjwa kutoka zahanati kumi na moja(11) , za wilaya ya Bahi na Wilaya jirani ya Chemba.

“Kituo cha afya Mundemu kinapokea rufaa za wagojwa kutoka zahanati kumi na moja(11) za tarafa hii, zahanati mbili kutoka tarafa ya Bahi na hata rufaa kutoka Wilaya jirani ya Chemba ambao huja kuhudumiwa katika kituo hiki” alisema Mhimbira.

Kituo cha afya Mundemu, ni moja ya vituo vilivyofaidika na mpango wa serikali wa kupanua kuwa na hadhi ambapo kilipokea milioni mia tano,(5000,000,000), ambazo zilitumika kuongeza majengo matano, ambayo ni jingo la jingo la mama na mtoto, maabara, jengo la upasuaji, nyumba ya Daktari, mochwari na kichomeo cha taka.

Katika kituo hicho, Mganga mkuu amebainisha kuwa kuna changamoto katika ujenzi wa njia za kuunganisha majengo na eneo la mochari alibainisha kuwa milioni tano zimetengwa kwa ajiri ya njia za kuunganisha majengo ya hospitali, na Mbunge aliahidi pindi wakianza ujenzi wa njia ya kuunganisha na Mochwari atachangia. ujenzi huo.

Pia wamekagua ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Chonde, ambao waliamua kujenga zahanati baada ya kufuata huduma ya afya kwa umbali mrefu takribani kilimita saba 7, hivyo wakaanza ujenzi wa zahanati ujenzi ulianza mwaka 2007, kwa nguvu za wananchi, na mpaka sasa ujenzi upo katika ngazi ya kuezekwa na umegharimu milioni therathini na saba laki saba na sabini elfu(37,770,000), kwa nguvu za wananchi, na Mbunge wa jimbo la Bahi na wadau mbalimbali.

Pia wametembelea shule ya sekondari ya Chonama, iliyopo katika kijiji cha Makanda ambapo mkuu wa Shule hiyo Henerietha Kahumuliza, amesema shule huyo alianzishwa 2009, Na inawanafunzi mia moja ishirini na tano, 125 inahudumia vijiji viwili Chonde na Makanda, kitaaluma inafanya vizuri kiwilaya inaongoza kila mwaka na kimkoa inashika nafasi 6 za juu.

Amesema Shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchache wa madarasa, haina maabara, na nyumba za walimu, changamoto kubwa ni Mabweni kwani kuna watoto wanaosoma umbali mrefu hutembea kilimita 14 kila siku, ambapo Mbunge Mariam Ditopile katika kuunga mkono amechangia kiasi cha sh. Laki tano(500,000) kwa ajiri ya kuendelea na ujenzi wa madarasa.

Katika ziara hiyo kamati ya utekelezaji ya UVCCM, imetembelea ujenzi wa zahanati ya Chonde, shule ya sekondari Chonama, Zahanati ya Makanda na mradi wa kilimo wa LUBALA SACCOS.

No comments