Breaking News

MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA AFYA, BARABARA KM 202.5MTWARA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akizungumza na wananchi wa Masasi mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Mbonde kilichopo Masasi mkoani Mtwara.

Dkt. Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakati akikagua moja ya Wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kukifungua Masasi mkoani Mtwara.

Sehemu ya Wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kufunguliwa na Dkt. Magufuli Masasi mkoani Mtwara.

Dkt. Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara, wakati akikagua chumba cha upasuaji katika wodi ya Wazazi katika  Kituo cha Afya cha Mbonde Masasi mkoani Mtwara.

Dkt. Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa wa Mtwara akiangalia mashine ya kutoa dawa ya usingizi kkwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji kwa wa mama wajawazito.

Sehemu ya wakazi wa Masasi wakisikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli wakati akihutubia mara baada ya kufungua kituo cha afya cha Mbonde.

Dkt. Magufuli akiwapungua mkono wananchi hawaonekani pichani wakati akiondoka eneo la kituo cha Afya cha Mbonde.

Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Mbonde mara baada ya kukifungua.

Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mikangaula iliyopo Nanyumbu mkoani Mtwara wakati akielekea Mangaka kwenda kufungua barabara.


Dkt. Magufuli akiwasalimia wananchi wa Nanyumbu mara baada ya kuwasili kutoka Masasi kwa ajili ya kufungua barabara ya Tunduru-Mangaka-Mtambaswala yenye jumla ya km202.5.PICHA NA IKULU

No comments