Breaking News

MAGUFULI AIONGEZEA MUDA TTB.

Rais Dkt. John Magufuli ameongeza muda wa miaka 3 kwa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iliyokuwa imalize muda wake leo tarehe 23 Aprili, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa bodi hiyo  wameongezewa muda hadi tarehe 23 Aprili, 2022.

Bodi hiyo inaongozwa na Mwenyekiti, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na wajumbe 6 kama ifuatavyo, Augustine Kungu Olal,  Zabein Muhaji Mhita, Richard Rugimbana, Mark Leveri, Ally Hussein Laay, Ibrahim Mussa

No comments