Breaking News

MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA AFYA MADABA MKOANI RUVUMA.


Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akizungumza na wanachi wa Kijiji cha Mageuzi Wilaya ya Namtumbo wakati akiwa njiani kuelekea Madaba mkoani Ruvuma, Ambapo amechangia Shilingi Milioni nane kwa Shule ya Msingi na Sekondari Mageuzi.


Dkt. Magufuli akizungumza na Wakazi wa kijiji cha Ndelenyuma ambapo awali kilikuwa ni kitongoji na sasa ametangaza rasmi kuwa kijiji alipokuwa akielekea Madaba mkoani Ruvuma kwenye uzinduzi wa kituo cha Afya Madaba.

 
Dkt. Magufuli akiwa na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen pamoja na wadau wa Maendeleo wakifunua kitambaa kuashiria Uzinduzi rasmi wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.


Dkt. Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen pamoja na wadau wa Maendeleo wakipiga makofi mara baada ya kufunua kitambaa kuashiria Uzinduzi rasmi wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.

 
Dkt. Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen,Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli pamoja na wadau wa Maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.

 
John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu , Mama Janeth Magufuli pamoja na Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen, Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli pamoja na wadau wa Maendeleo wakifurahi mara baada ya kuzindua wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.

 
Dkt. Magufuli akikata utepe pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Denmark nchini  Heinar Jensen,Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli pamoja na wadau wa Maendeleo kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.

 
Dkt. Magufuli akiwa ameshikana mikono pamoja na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen, Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Mhe.Frolence Mattli, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja pamoja na wadau wa Maendeleo alipokuwa akikagua Wodi ya Wazazi ya  Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.

 
Dkt. Magufuli akiagua kitanda cha kujifungulia katika Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua kituo hicho.

 
Dkt. Magufuli akiagua Vitanda katika Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua kituo hicho.


 
Dkt. Magufuli akiagua Vifaa katika Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua kituo hicho.

 
Dkt. Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen, Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na wadau wa Maendeleo wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za uzinduzi wa  Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.

 PICHA NA IKULU

No comments