Breaking News

MAGUFULI AZINDUA MRADI WA UMEME KUTOKA MAKAMBAKO HADI SONGEA.

Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakiminya kitufe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.

Dkt. Magufuli akimshukuru Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg mara baada ya uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu wa umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.
Dkt. Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakiangalia mradi huo wa umeme utakavyosambaza umeme katika maeneo mbalimbali kutoka kutoka Makambako hadi Songea

Dkt. Magufuli akiwa na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg, Waziri wa Nishati Medard Kalemani wakielekea eneo la uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa usafirishaji wa umeme.
Dkt. Magufuli akiwa na Balozi wa Sweden hapa nchini Anders Sjoberg wakipungia mikono wananchi waliohudhuria katika sherehe hizo za uzinduzi wa mradi wa umeme.

Dkt. Magufuli akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa mradi wa Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme KV 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na vituo vya kupooza umeme KV 220/33  katika sherehe zilizofanyika Songea mkoani Ruvuma.

Moja ya kituo cha kupooza umeme cha Songea.


Dkt. Magufuli akizindua kituo Kikuu cha Mabasi cha Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Dkt. Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo Kikuu cha Mabasi cha Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Sehemu ya wananchi wa Songea mkoani Ruvuma wakiwa ndani ya Uwanja wa mpira wa Majimaji kumsikiliza Dkt. Magufuli. PICHA NA IKULU


No comments