Breaking News

MATUMIZI MIFUKO YA PLASTIC MWISHO MWAKA HUU.

Na Furaha John, Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira  January Makamba amesema katika bajeti ya wizara hiyo ya mwaka huu serikali huenda wakatangaza kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki nchini ifikapo Julai Mosi kuwa mwisho.

Makamba ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Kaliua Magdalena Sakaya.

Katika swali hilo Sakaya ametaka kujua kama serikali haioni kuwa inaendelea kulinda matumizi ya mifuko hiyo Kwa kuacha ikiendelea kutumika maeneo yote nchini.

Akijibu swali hilo Makamba amesema tayari alishapokea maelekezo kutoka kwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa  ya kukutana na taasisi za serikali zinazohusika na jambo hilo kama NEMC, ili kuona namna wanavyoweza kupiga marufuku na tayari kanuni zipo anatarajia kuzitangaza kwenye gazeti la serikali.

Awali katika swali la msingi mbunge huyo ametaka kujua serikali ina mikakati gani ya kuondoa matumizi ya plastick hapa nchini.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa wizara hiyo Mussa Sima ametaja hatua zilizoanza kuchukuliwa kuwa ni pamoja na  kuhamasisha wajasiriamali, vikundi vya akina mama na vijana, sekta binafsi na viwanda kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala ikiwemo vikapu vya asili, mifuko ya karatasi na vitambaa.

No comments