Breaking News

MUROTO:ACT WAZALENDO WAKIANDAMANA JIJINI DODOMA 'WATAPIGWA WATACHAKAA'Na.Alex Mathias,Dodoma
Chama cha ACT Wazalendo pamoja na baadhi ya vyama wameungana  kwa lengo la kufanya maandamano siku ya juma nne April 9, mwaka huu lakini tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema limejipanga kukabiliana na waandamanaji hao na iwapo watajitokeza watapigwa mkapa watachakaa.
 
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari,   amesema kupitia mitandao ya kijamii kuna taarifa za ACT Wazalendo kutaka kufanya maandamano kwa kushirikiana na baadhi ya vyama vingine kikiwemo Chama cha NCCR-Mageuzi.
 
"ACT Wazalendo wanakusudia kufanya maandamano kesho yaani Apirili 9,2019. Nataka kuwaambia hao wanaotangaza maandamano kwa njia ya mtandao wakiingia barabarani kama ni kweli watapigwa watachaa.Narudia tena watapigwa watachakaa,"amesema Kamanda Muroto .
 
Amefafanua Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa sasa linaendelea na mazoezi na lipo tayari kukabiliana na wandamanaji, hivyo wanawasubiri kwa hamu kama wapo huku akifafanua maandamano hayo ni haramu na hayapaswi kufanyika.
 
"Wananchi wa Mkoa wa Dodoma msiwe na wasiwasi, endeleeni na shughuli zenu kama kawaida na wabunge nao waendelee na vikao vya Bunge.Polisi tumejipanga na tuko tayari,"amesema Kamanda Muroto na kusisitiza watakaondamana hiyo kesho watapigwa watachaa.

 ACT Wazalendo walitangaza kufanyika kwa maandamano hayo ikiwa ni sehemu ya kuonesha hisia zao za kutofurahishwa na uamuzi wa Bunge la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Profesa Mussa Assad

No comments