Breaking News

MWAMKO WA JAMII KATIKA ELIMU BADO NI CHANGAMOTO:DITOPILE


Na EZEKIEL NASHON, BAHI.

Licha ya Serikali kuelekeza nguvu nyingi katika sekta elimu imeelezwa kuwa bado kuna mwamuko mdogo wa jamii  katika maswala ya elimu.

Hayo yameibuliwa  na Mbunge wa viti maalumu anayewakilisha kundi la vijana, Mariam Ditopile, wakati wa Ziara ya kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi, UVCCM, Mkoa wa Dodoma, katika kata ya Mwitikira, Wilayani Bahi.

Walipotembelea shule ya sekondari Mwitikira ikiwa ni kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama, alisema serikali imewekeza nguvu nyingi lakini mwamko wa jamii katika kuthamini elimu bado ni mdogo hali inayopelekea kutofikia malengo, ya kutoa elimu bora.

“Sitaki  nitumie lugha kali ninachotaka kusema bado kuna mwamko mdogo wa jamii katika kuthamini elimu sijui watu hawaamini kuwa elimu inaweza kuwa komboa! licha ya kusikia kwa mwalimu juhudi zilizofanywa na serikali ya kutoa elimu bure, watu tangu msingi”,

“Tunaona Rais  anafanya jitihada kubwa, na hasa hili la kuhamishia makao makuu, inaenda na fursa ya vyuo vikuu vilivyopo hapa vitaangaliwa kwa jicho la tofauti, sitaki nionekane mbaguzi lakini ukweli vyuo hivi vilitakiwa viwafaidishe wana Dodoma, vyuo kama Udom, Hombolo na Mipango watatoka wataalamu lakini watasambaa”, alisema  Mariam.

Amesema Serikali ilichukua jukumu la kusomesha kutoka elimu ya msingi hadi  kidato cha nne, lakini suala la kukagua maendeleo ya mwanafunzi sio jukumu la Serikali tena ni jukumu la mzazi, kuhakikisha mtoto anasoma na kukagua maendeleo ya mtoto  awapo shule na jukumu la serikali ni kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya mwanafunzi kusoma.

Aidha amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zote waone haja ya kusimamia suala la elimu kwani swala hili ni shirikishi kwa maendeleo ya nchi yetu, na ili kuhakikisha hili linatimia wana ccm na jumuiya zake zote wahakikishe wanachukua jukumu la kusaidia katika suala la elimu.

Amefikia uamuzi huo  baada ya kupokea  ripoti  ya shule ya sekondari Mwitikira kwa makamu wa shule, Hamis Sang’wa, kuwa shule hiyo inamatokea mabaya kitaaluma na kueleza kuwa chanzo ni utoro wa wanafunzi katika shule hiyo ambayo yanapelekea matokeo mabaya kitaaluma.

Amesema baada ya kubaini hilo tayari wameanza kulifanyia kazi, ambapo walibaini kuwa watoto  wakiwa nyumbani hawasomi hali inayopelekea kuwa na matokeo mabaya na sasa wameanzisha mpango wa kuwaweka shule kidato cha pili na nne wanakaa shule ili kuona namna ya kuipandisha shule kitaaluma.

Katika ziara hiyo kamati ya utekelezaji ya UVCCM, ilitembelea ujenzi wa madarasa na mabweni, katika shule ya sekondari Mwitikira, ambapo huko kamati ilipokea taarifa kwa makamu mkuu wa shule hiyo, Hamis Sang’wa.

Amesema shule  hiyo inawanafunzi 206,  kidato cha kwanza hadi  cha nne, shule hiyo ilipokea milioni mia  moja na  kumi na tano,(115,000,000), ikiwa milioni arobaini(40,000,000) kwa ajiri ya Madarasa, na milioni sabini na tano(75,000,000) kwa ajiri ya ujenzi wa Mabweni.

Pia kamati imetembelea katika  kiwanda cha MGWABI INVESTIMENT COMPANY, ambaye anazalisha wine, kiwanda kilianza mwaka 2016,  akianzia shughuri zake kwa kutumia mikono,  lakini baada ya umeme kufika katika kiwanda hicho, alinunua mashine za kuzalisha Wine.

Amebainisha kina wafanya kazi wanne, na kinasubiri nembo ya TBS, ilikiweze kuanza kuuza bidhaa zake, na sasa kipo hatua za mwisho kupata nembo ya TBS, pia mwaka 2016 aliweza kupata tuzo ya mkulima bora wa kanda ya kati.

Diwani wa kata hiyo  Danford Chisomi, amebainisha wameanzisha ujenzi wa ofisi ya chama ya kata na kwa kuanza yeye  mwenyewe ametoa tofari elfu moja(1000), ambapo Mbunge Mariam Ditopile, aliahidi kutoa mifuko 20 ya saruji kwa ajiri ya ujenzi wa Ofisi ya Chama, na ikikamilika atatoa Computer  na Printer zitumike katika  ofisi ya chama.

Pia ameahidi kumpa baiskeli katibu wa kata ya Mwitikira Eudia Lukowe, anayehudumia vijiji vingi hivyo baiskeli itamsaidia katika majukumu yake ya kila siku, pia alitoa mifuko kumi (10) ya saruji na laki mbili(200,000) ya mbao za kuezekea madarasa katika kijiji cha Mapanga.

No comments