Breaking News

SAKATA LA CAG LAMUIBUA MNYIKA NA CHENGE.


Na Furaha John, Dodoma

MWENYEKITI wa Bunge, Andrew Chenge amesema Serikali haijaenda nje ya utaratibu unaotakiwa kuhusu uwasilishwaji wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) huku akimtaka Mbunge wa Kibamba John Mnyika(Chadema) kusoma upya Katiba na sheria.

Chenge ametoa kauli hiyo  kufuatia mwongozo alioomba Mbunge huyo jana mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na utambulisho wa wageni mbalimbali uliofanywa na Naibu Spika Tulia Ackson lakini baadae alimpisha Chenge.

“Nakusihi sana uende ukasome sheria ya tafsiri inapoeleza siku. Serikali haijaenda nje ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa katiba,”alisema.
Kupitia mongozo wake Mnyika amesema "Mapema leo asubuhi tumekabidhiwa orodha ya shughuli za leo ambayo pamoja na mambo mengine kulikuwa na hati ya kuwasilisha mezani.
"Lakini Mwenyekiti, katiba ya nchi ibara ya 143 ibara ndogo ya 4 inasma mdhibiti naa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atawasilisha kwa rais kila taarifa itakayotoa kwa mujibu wa masharti ya ibara dogo ya pili," amesema.
Mnyika amefafanua kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo rais atawaagiza watu wanaohusika wakaiwasilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha bunge kitakachofanyika baada ya rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla haijapita siku saba tangu siku iliyoanza kikao hicho.
Pia amehoji, kama rais hatochukua hatua ya kuwasilisha taarifa hiyo kwenye bunge basi mdhibiti na mkaguzi mkuu atawasilisha taarifa hiyo kwa spika wa bunge au naibu spika ikiwa kiti cha spika kiko wazi au ikiwa kwa sababu zozote spika hawezi kuwatekezeza shughuli zake basi ataiwasilisha taarifa hiyo kwenye bunge.
Mbunge huyo katika muongozo wake ameeleza kwamba taarifa iliyotolewa na ofisi ya  CAG inaonyesha kwamba Machi 28 rais alipokea ripoti za ukaguzi kutoka kwa CAG kwa mwaka wa fedha unaoishia June 2018.
Ametanabaisha kuwa kikao cha kwanza cha bunge kilianza tarehe mbili ya mwezi huu ambapo taarifa alizopokea rais hazijawasilishwa na katiba imezungumzia siku saba haijazungumzia siku za kazi au zisizokuwa za kazi.
Baada ya Mbunge huyo, kuomba mwongozo huo, Mnadhimu Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Jenista Mhagama akasimama na kuomba kutoa taarifa.
Jenista katika taarifa yake amenukuu vifungu vya sheria ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali lakini hakwenda mbali zaidi kusoma sheria zingine zinazoambatana na maagizo hayo ya kikatiba na sheria katika kufanya tafsiri za siku ambazo zimeandikwa kwenye katiba na sheria husika na uwasilishaji wa ripoti ya CAG na hasa sheria ya tafsiri ya sheria.
Mnadhimu huyo amefafanua kuwa mbunge anataka kuonyesha wazi kama serikali haitaki kuwajibika huku akimuomba mwongozo wa mwenyekiti linapotokea jambo kama hilo endapo kiti kipo tayari kumtafsiria myika tasfiri ya sheria hizo zote ili asiendeleee kulipotosha bunge na akatuacha serikali tuendelee kujipanga kwa kuzingatia sheria na taratibu husika katika utekelezaji wa jambo hili.
Baada ya maelezo hayo, Mwenyekiti wa kikao hicho, Chenge alifafanua kuwa katiba lazima isomwe na kutafsiriwa vizuri.
”Katiba kama ulivyoisoma lazima uisome na sheria nyingine na sheria moja inayotuongoza ni sheria ya tafsiri za maneno yote ambayo yametumika kwenye sheria, sura namba moja ndio inayoumika,"amesema.
Ameeleza kuwa kauli ya kuwa halikutokea kwenye orodha ya shughuli za bunge ’order papaer’ hakuna kitu kama hicho.
Pia amemsii na kumtaka Mnyika aende ukasome sheria ya tafsiri inapoeleza siku, na kusisiriza kuwa Serikali haijaenda nje ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa katiba ya nchi.


No comments