Breaking News

TUMSAIDIE MKULIMA KUONGEZA TIJA - BASHUNGWA.


Na.Alex Mathias,Dodoma

NAIBU WAZIRI wa Kilimo, Innocent Bashungwa amewataka Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) na Viongozi wa Bodi za Mazao kuweka Mkakati wa Pamoja wa kumsaidia Mkulima ili kuongeza tija katika uzalishaji na uuzaji wa mazao .
  
Hayo ameyasema  leo jijini Dodoma wakati akifungua  Kikao Kazi cha Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) na viongozi wa bodi za mazao ambapo amesema kuwa wanatakiwa kumsaidia mkulima kupata pembejeo ambayo itaweza kumsaiadia katika kuzalisha mazao bora.

“Hakikisheni mnakuwa na Mkakati wa Pamoja wa Upatikanaji wa pembejeo, uhakika wa masoko na namna bora ya kuhifadhi mazao ya wakulima ikiwemo ujenzi wa maghala,” amesema Bashungwa.  

Aidha, amesema kuwa  Mfumo wa Ushirika ukitumika vizuri utawasaidia wananchi kupata masoko ya mazao yao ndani na nje ya nchi na ameitaka Tume  ya Maendeleo ya Ushirika na Bodi za Mazao kutafuta masoko ya bidhaa za wakulima na kuacha kuwategemea Viongozi wa juu wa Serikali kuingilia katikati kutatua changamoto za wakulima.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Titus Kamani amesema kuwa lengo la kikao hicho ni Kutafsiri kwa pamoja ujenzi na uchumi wa kilimo kupitia dhana ya ushirika na kuondoa  mazingira ya migogoro inayojitokeza ili kuepuka kujitokeza tena ukizingatia kuwa Bodi za Mazao na Ushirika ni wadau muhimu.

“Tumeona juhudi zinazofanywa na Serikali katika kumsaidia mkulima kunufaika na shughuli zake za kilimo kupitia sekta ya Ushirika na mabadiliko kwa baadhi ya maeneo  japo kuwa bado kuna changamoto,” amesema Dkt. Kamani.

Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania amehimiza upatikanaji wa masoko bora kuhakikisha mazao yote ya kimkakati na yale yasiyo ya kimkakati yanaingizwa pamoja na Mfumo wa Stakabadhi za Ghala,  Mfumo wa Soko la Bidhaa na mingine kulingana na aina zao na mfumo wa biashara ulivyo


No comments