Breaking News

UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA DODODMA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la Mama na Mtoto katika Hospitali hiyo.

Ummy Mwalimu (kushoto) akiongea jambo wakati alipofanya ziara ya kukagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General). Kulia ni katibu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula.

Ummy Mwalimu (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula wakiangalia kitu katika wodi ya akinamama waliojifungua wakati walipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo jipya la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
 
Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula wakifurahia jambo wakati wanasaini kitabu cha wageni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati walipofanya ziara ya kukagua jengo la mama na mtoto.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea hotuba kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Benzi wakati walipofanya ziara ya kukagua jengo la mama na mtoto (Maternity Block). Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na nyuma  viongozi we gongine wa Wizara na Hospitali.

 Jengo jipya la Mama na Mtoto (Maternity Block) lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

No comments