Breaking News

WACHIMBAJI WATELEKEZA MADINI NA PIKIPIKI NA KUKIMBIA.


 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Kikula wa pili kushoto akiangalia madini ya Rubi Nut yaliyotelekezwa na mchimbaji wa madini hayo Sadick Athuman maarufu kwa jina la Saadam alie kimbia baada ya kuona msafara wa tume ya Madini na Mkuu wa Wilaya Gairo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya Gairo Siriel Shaid Mchembe na Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke.
 
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Kikula wa pili kulia akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya gairo ikiongozwa na mwenyekiti wake Siriel Mchembe wa tatu kushoto na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke wakionyesha baadhi ya vifaa ikiwemo pikipiki iliyo telekezwa na  mchimbaji wa madini Sadick Athuman maarufu kwa jina la Saadam alie kimbia baada ya kuona msafara wa tume ya Madini.
 
Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas  Machiyeke mwenye kofia ya blue na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na viongozi mbalimbali wakifanya jitihada ya kuinasua Gari ya polisi iliyokuwa imenaswa kwenye maji katikati ya mto wakati wakielekea mgodini.
 
Msafara wa tume ya Madini na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwa kwenye eneo la mgodi Kijiji cha Kirama walipotembelea kukagua shuguli za uchimbaji katika eneo hilo wa mbele ni Athumani anae uongoza msafara kwenda kuonyesha anapochimba Sadick Athuan baada ya kukimbia

Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mwenyekiti wa Tume ya Madini na Kamishna wa Tume ya Madini na mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiangalia aina ya mawe yenye asili ya madini ambayo yameokotwa juu ya ardhi kwenye shamba la mahindi kandokando ya mto.
 
Kamanda wa jeshi la wananchi “Sajenti” Mkongwa akijaribu kuiwasha pikipiki iliyotelekezwa na mchimbaji wa madini Sadick Athumani baada ya kuona msafara wa tume ya madini na kamati ya ulinzi na usalama.
 
Dkt. Machiyeke akifukia shimo barabarani ili kuwezesha magari yapite yaliyo kuwa yanaelekea mgodini kwa kwa lengo la kwenda kukagua shuguli za uchimbaji, mwenye sakafu ni mkuu wa wilaya ya Gairo na mwenye sare nyeupe ni askari wa usalama barabarani wilaya ya Gairo Sarehe Rajabu Mkambaku.


No comments