Breaking News

WANAFUNZI SEKONDARY WAFANYA ZIARA CHUO KIKUU UDSM.


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Arnold Towo akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mt. John Paul II ya Kahama Mkoani Shinyanga walipofanya ziara ya masomo kwa vitendo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam tarehe 12 Aprili, 2019.   

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mt. John Paul II ya Kahama Mkoani Shinyanga wakisikiliza kwa makini kuhusu huduma zinazotolewa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati wa ziara waliyofanya katika Kitengo cha Huduma kwa Umma.

Elizabeth Chuwa kutoka Kurugenzi ya Masomo ya Shahada ya Awali akiwaeleza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul taratibu za kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es salaam wakati wa ziara fupi iliyofanywa na shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo katika Kitengo cha Huduma kwa Umma cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Kifaa cha Kisasa cha Kutunzia kadi za Kielektroniki ( Electronic Cabinet ) chenye kadi 170 kilichopo katika Maktaba Mpya ya Kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mwandamizi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ernest Nyari akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul ya Kahama namna kabati la Kielektroniki linavyotumiwa na wanafunzi wanapoingia Maktaba wakati wa kujisomea.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul wa II wakiwa wamekaa ndani ya chumba kisasa cha taarifa za mtandaoni " Online Publications" wakati wa ziara fupi ya masomo kwa vitendo iliyofanywa na shule hiyo katika Kitengo cha Huduma kwa Umma cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Msaidizi wa Maktaba Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Dickens Dominic akiwafafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya John Paul II wakati wa ziara ya kimasomo waliyofanya kujionea namna Maktaba mpya inavyofanyakazi.

Mkurugenzi Mwandamizi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ernest Nyari akiwaonesha wanafunzi (Hawapo pichani) moja ya Vitabu vya Sayansi vinavyopatikana katika chumba cha Maktaba mahususi kwa ajili ya masomo ya Sayansi kiitwacho " Science Collection" wakati wa ziara fupi iliyofanywa na shule ya Sekondari ya Mt. John Paul II katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma ( Mwenye shati la Bluu) pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitengo cha Huduma kwa Umma na Maktaba Mpya wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul II kutoka Kahama Shinyanga baada ya ziara fupi katika Maktaba hiyo.

No comments