Breaking News

WATAALAMU WA TAFITI ZA MIFUGO WATAKIWA KUJIKITA KATIKA MFUMO WA UZALISHAJI KIUCHUMI.


MSAJILI wa Baraza la Veterinari nchini Dkt. Bedan Masuruli  ametoa wito kwa wataalamu wanaofanya Tafiti za Mifugo kuangalia kwa kina na kuweka mikakati stahiki katika mfumo wa uzalishaji kiuchumi pamoja na kuongeza nguvu  katika mnyororo wa thamani.

Dkt.Masuruli  ameyasema hayo leo jijini hapa  wakati akifungua kikao cha wadau wa sekta ya mifugo cha kuhuisha agenda ya utafiti wa mifugo nchini.

Naye Mkurugenzi wa Utafiti wa Mafunzo na Ugani Dkt. Mwilawa amesema kuwa timu za wataalamu kutoka Idara ya Utafiti na Mafunzo ya wizara pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) kwa pamoja  zilishirikisha mawazo ya kutengeneza rasimu ambayo italenga kuleta malengo mapya  imelenga kufika  kitaifa. 

Kwa upande wake Katibu wa Mkuu Chama cha Wafugaji nchini   Magembe Makoye ameeleza kuwaa umeibuka mtindo katika jamii wa kudharau utaalamu uanofanywa na watafiti.


No comments