Breaking News

UTOVU WA NIDHAMU WAMUADHIBU MAKAMU WA BUNGE LA AFRIKA.Na Furaha John, Dodoma

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amemsimamisha kwa muda mwakilishi wa Tanzania ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Bunge la Afrika Stephen Masele kwa  tuhuma za utovu wa nidhamu.

Akitoa taarifa Bungeni Dodoma leo Spika  amesema amemwandikia barua Masele, ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga Mjini(CCM), kurudi nchini kuhojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, pamoja na Kamati ya Usalama na Maadili  ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Katika hatua Nyingine Spika amelitaarifu Bunge kwamba amepokea ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu wa Ofisi ya Taifa  ya Ukaguzi kutoka Kwa kampuni ya ukaguzi  ya E.K Mangesho and Company, kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2018.

Amesema baada ya kupokea ripoti hiyo ameiwasilisha Kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) Kwa uchambuzi.

“Kamati ikishakamilisha Kazi ya kuchambua na kupitia ripoti hiyo, watairejesha kwangu Kwa hatua zaidi,”amesema Spika.

Pia amesisitiza kuwa katika ukaguzi  huo hakuna atakayebaki kila  anayehusika atafanyiwa kazi.

 “ Kwa mujibu wa kifungu 46 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya ukaguzi wa Umma sheria namba 11 ya mwaka 2008, hesabu za CAG yaani za ofisi ya taifa ya ukaguzi zinapaswa kukaguliwa angalau mara moja kwa mwaka na kwamba Bunge kupitia kamati ya kudumu ya Hesabu za serikali (PAC) uwa ina jukumu la kuteua mkaguzi wa kukagua hesabu za ofisi hiyo, kwa maneno rahisi bunge ndio tunatafuta mkaguzi wa nje ambaye ndiye anayekagua hesabu za CAG,”amesema. 

Ndugai amefafanua kuwa, ameona ni muhimu kuwajulisha ili waweze kufahamu katika hesabu zilizowekwa mezani kwa wakati muafaka.

No comments