Breaking News

MHE. IKUPA ATOA MSAADA WA BAISKELI KWA MTOTO WENYE ULEMAVU.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Stella Ikupa akieleza jambo kuhusu umuhimu wa kuwajali Watu wenye Ulemavu wakati alipokuwa akitoamsaada wa baiskeli kwa mtoto Happy Shabani Salumu wenye Ulemavu, Jijini Dodoma Mei 15, 2019.

Naibu Waziri, Stella Ikupa akizungumza na mzazi wa mtoto huyo Magreth Leo alipokuwa akitoa msaada wa baiskeli.

Magreth Leo (katikati) akimwelezea jambo Naibu Waziri, Stella Ikupa (kushoto) kuhusu mtoto wake Happy Shabani Salumu wenye Ulemavu. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu Josephine Lyengi.


Baadhi ya Maafisa wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu wakifuatilia maelezo ya Naibu Waziri, Stella Ikupa (hayupo pichani) alipokuwa akitoa msaada wa baiskeli kwa mtoto Happy Shabani Salumu. Kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii Joy Maongezi na Oliver Njogopa (katikati).

Naibu Waziri, Stella Ikupa akimkabidhi baiskeli mtoto Happy Shabani Salumu, ambaye ni mlemavu wa viungo itakayo msaidia kwenda shuleni na kumwezesha kufanya shughuli nyingine kwa urahisi. Kulia ni Mzazi wa mtoto huyo Bi. Magreth Leo.

Naibu Waziri, Stella Ikupa akifurahi pamoja na mzazi wa mtoto huyo Magreth Leo alipomkabidhi fedha kwa ajili ya matibabu ya mtoto Happy Shabani Salumu wenye Ulemavu.

Naibu Waziri, Stella Ikupa akiwa na mtoto mwenye Ulemavu Happy Shabani Salumu mara baada ya kukabidi msaada wa baiskeli kwa mtoto huyo Mei 15, 2019 Jijini Dodoma.

No comments