Breaking News

JPM AZUNGUMZA NA WAKAZI WA MAENEO TOFAUTI MKOANI KAGERA.

Dkt. John Magufuli akizungumza na wananchi wa Rwamishenye wakati akitokea Karagwe mkoani Kagera.


Dkt. Magufuli akiandika kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wananchi wa Muleba mkoani Kagera wakati akielekea Chato mkoani Geita.


Dkt. Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Muleba Mjini mkoani Kagera wakati walipokuwa wakielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili.


Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape akiwa pamoja na wananchi wa Rwamishenye wakifurahia wakati wakimsikiliza Rais Dkt. Magufuli wakati aliposimama katika eneo hilo na kuwasalimu.


Dkt. Magufuli akisalimiana na Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape katika eneo hilo la Rwamishenye wakati akielekea Chato mkoani Geita.


Dkt. Magufuli akiombewa na Mtume Venon Fernandes wa Kanisa la Agape pamoja na wananchi wa Rwamishenye Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuzungumza nao wakati akitokea Karagwe.Dkt. Magufuli akizungumza na wananchi wa Kemondo nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.


Dkt. Magufuli akiondoka katika eneo la Muleba mjini mara baada ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.


Dkt. Magufuli akisali mbele ya Kaburi la Marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu kutoka Wizara ya Ujenzi.


Dkt. Magufuli akizungumza nyumbani kwa marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu kutoka Wizara ya Ujenzi mara baada ya kuwasili kijijini hapo Muleba mkoani Kagera. Marehemu Mhandisi Mjungi alifariki mwaka 2007.


Dkt. Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Muleba wakati akitoka nyumbani kwa marehemu Mhandisi Leopard Mjungi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa barabara Kuu wa Wizara ya Ujenzi. Picha na Ikulu.

No comments