Breaking News

WATANZANIA WATAKIWA KUACHA WOGA KUJENGA VIWANDA VIDOGO NA VYA KATI.


 

WATANZANIA wametakiwa kuacha woga kuwekeza katika ujenzi wa viwanda kama kweli wanataka kupata maendeleo ya haraka kama zilivyo nchi za Ulaya.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa BIGTEM TANZANIA & FEMIA Bob Yona katika maonesho ya 43 maarufu kama sabasaba Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema ifike wakati kwa watanzania wengi zaidi kumiliki viwanda kama ilivyo ilani ya chama cha mapinduzi ya kuhakikisha Tanzania inajenga viwanda vya kutosha.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa katika maonesho ya sabasaba kampuni yake imeleta mashine za iwandani aina mbalimbali kubwa na ndogo ili kumpa nafasi kila mtanzania kumiliki kiwanda kutokana na mahitaji katika eneo, kuna mashine za kuchakata matunda kama vile machungwa, machenza, maembo, mbogamboga na mazao ya nafaka mchanganyiko.

Yona amesema Tanzania inategemea zaidi sekta ya Kilimo katika kukuza uchumi na katika eneo hili kuna ajira nyingi kuliko eneo linguine.

“Serikali imeweka juhudi kubwa sana katika kuhamasisha ujenzi wa viwanda na ndio maana kampuni yetu ikaona kuna umuhimu kuja sabasaba kuonesha aina hizi za mashine na kuwataka wananchi wafike kuangalia au kuuliza kitu chochote maana wengi wanapita tu.” Amesema.

Amesema Watanzania wanaogopa hata kuuliza ubora wa mashine, hivyo amewataka kufika kuangalia aina mbalimbali na kuwataka wasihofie bei maana kila mmoja anaweza kumiliki kutokana na utaratibu uliowekwa na kampuni.

Ameyapongeza maonesho hayo ambayo yamewafanya watanzania kukutana pamoja na kuzungumza lugha moja ya biashara na kuhamasisha mwaka ujao maonesho yaimarishwe zaidi na kuongeza vivutio ikiwa ni pamoja na kupunguza bei za viingilio kwa wananchi ili wengi wapate nafasi ya kuingia kujifunza

No comments