Breaking News

KUHUSU VIDEO ZA UTUPU ;DIAMOND NA NANDY WAOMBA RADHI


NA MWANDISHI WETU
Mwanamuziki nyota nchini Tanzania, Naseeb Abdul maarufu Diamod Platnumz na Faustina Charles, maarufu Nandi wamejitokeza hadharani kuomba radhi kutokana na kitendo cha kupiga picha zinazodaiwa kuwa 'chafu' picha ambazo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii juma lililopita.
Kusambaa kwa picha hizo kulizusha ghadhabu mitandaoni huku wawili hao wakinyooshewa kidole kwa kile kinachodaiwa kuvunja maadili na sheria za Tanzania.
Katika mazungumzo na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, kwenye Ofisi za mamlaka ya mawasiliano Tanzania Diamond alikiri kufanya makosa na kuomba radhi.
"Kuna clip ambazo zimekuwepo na zinanihusu ambazo hazikuwa nzuri ki ukweli. Pengine katika tamaduni za zamani tungeona kama baridi tu lakini sasa kwa kanuni hizi ..basi tuziache na tufanye vitu vilivyokuwa vizuri na kwa mtu ambaye zilimkwaza pengine, tuvumiliane, tusameheane tu'', amesema Diamond.
Diamond amesema kutokana na kilichotokea amepata nafasi ya kujifunza kanuni mbali mbali na kuzifuata.
''Ikiwa serikali inatukingia kifua na kutuunga mkono tuhakikishe muziki wetu unafika mbali tukiwa tunaenda na tswira isiyo nzuri tunakuwa tunawavunja moyo viongozi ambao wanapambana kuhakikisha kuwa sanaa zetu zinafika mbali''. Alisema Mwanamuziki huyo.
Mapema wiki hii msanii huyo wa alihojiwa na maafisa wa polisi kwa video hiyo aliyoiweka kwenye mtandao wake wa Instagram.
Maafisa wanasema video hiyo imekosa maadili na inakiuka utamaduni wa Tanzania.
Mwanamuziki Nandi pia alikuwa kwenye mamlaka hiyo ya mawasiliano ameeleza hisia zake mbele ya waandishi baada ya tukio hilo ''nimefurahi kufika hapa na kupata elimu, nimejifunza kuwa sio sahihi kupiga picha za utupu kuweka mitandaoni, nimejutia sana kitendo kile tangu wakati huo kwa kuwa ilikuwa video ya faragha'' nilihuzunika baada ya video hiyo kutoka nje
Nandi amesema yuko tayari kuwaelimisha wengine hasa wasanii wenzake na vijana wanaotumia mitandao ya kijamii, ambao pia wamefanya vitendo kama vyake wakiwa faragha na kutoka hadharani.
Nandi ameomba radhi kwa mashabiki na wafuasi wake kutokana na athari zilizojitokeza baada ya video yake kusambaa mitandaoni, ''Ni kitu kilichoniumiza mimi , familia na mashabiki wangu''.
''haikuwa kusudio langu kutokea yaliyotokea''Alieleza.

No comments