Breaking News

LEA MIMBA KWA FASHENI KALI ZA NGUO

Lea mimba kwa fasheni kali za nguo 

NA MWANDISHI WETU 

KUWA mjamzito hakumfanyi mwanamke ashindwe kwenda na wakati, kuvaa nguo nzuri, kubeba pochi iliyobuniwa na wanamitindo maarufu duniani au kuvaa viatu vizuri.

Siku hizi huwezi kukuta mama mjamzito amevaa dera au gauni ambalo limekaa kihasarahasara, wajawazito wa sasa wanapendeza haswa. Zipo aina nyingi za nguo ambazo mwanamke mjamzito anaweza kuvaa katika kipindi chote ambacho analea mimba yake.

Miongoni mwa nguo hizo ni suruali za 'jeans' ambazo zimeshonwa maalum kwa ajili ya wanawake wajawazito, suruali hizo kiunoni zimeshonwa kwa kuwekewa kamba ambayo unaweza kufunga kulingana na ukumbwa wa mimba yako.Suruali hizo na aina nyingine za suruali zinapatikana kwenye maduka mengi nchini yanayouza nguo za wanawake wenye mimba.

Vazi lingine ambalo ni la kawaida ni kwa kila mjamzito ni gauni pana na la heshima kulingana na umri wa mimba.Magauni hayo yanaweza kuwa yameshonwa kwa kitambaa cha aina yeyote ile katika staili ambayo mvaaji atapenda kutokelezea.

Wengi wa wanawake wajawazito katika karne hii ya 21, wana mavazi mengine mengi ambayo huyabuni wao wenyewe kulingana na jinsi anayotaka yeye.


Wapo wanaovaa mashati makubwa yaliyofika usawa wa magoti na fulana pana ambazo ni kivutio kikubwa kwa wanawake wajawazito.

Aina hizi za mavazi na nyingine ambazo mvaaji anapenda kuvaa zinashauriwa kuwa za heshima ambazo haziachi tumbo wazi kwani kama mnavyojua sifa kubwa ya mama mjamzito ambaye umri wa mima yake ni mkubwa anapaswa kujisitiri yeye na mtoto wake.

No comments