Breaking News

PROFESA WANGARI ;MWAFRIKA WAKWANZA KUPATA TUZO YA NOBEL


Profesa Wangari

Mwanamke wa kwanza Mwafrika
kupewa tuzo ya Nobel

PROFESA Wangari Maathai ni mwanamke aliyejijengea umaarufu mkubwa duniani kutokana na utetezi wake wa haki za wanawake na mazingira.

Alizaliwa Aprili Mosi, 1940 katika Kijiji cha Ihithe wilaya ya Nyeri na familia yake ilikuwa  ya Kikuyu.


Mwaka 1943 baba yake ambaye alikuwa ni mfanyakazi alihamia katika mji w Nakuru. Familia hiyo ilikuwa maarufu sana nchini Kenya.

Profesa Wangari baada ya baba yake kufariki mwaka 1947, yeye na nduguze walirudi Ihithe na mama yake, kaka zake wawili ambao walikuwa wakisoma shule ya msingi vijijini ambako kulikuwa hakuna shule.

Hata hivyo, Profesa Wangari alivyofikisha umri wa miaka minane, aliungana na kaka zake shuleni ambako walikuwa wakisoma katika Shule ya Msingi Ihithe.

Pia, akiwa na umri wa miaka 11 alihamishiwa shule ya bweni ya ambayo ilikuwa ya Kanisa Katoliki ambayo ilikuwa Nyeri.

Profesa Wangari alisoma katika shule hiyo kwa muda wa miaka minne na alikimudu Kiingreza kwa ufasaha na mwaka 1956 alimaliza masomo yake.

Wangari alisomea elimu yake nchini Marekani pamoja na Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya na kutunukiwa tuzo hiyo mwaka 2004 kutokana na kazi zake alizokuwa akizifanya.

Mwanaharakati wa mazingira huyo katika miaka ya 80 na mshindi wa tuzo ya Nobel Profesa Wangari Maathai alifariki baada ya kuugua Saratani.

Katika miaka ya 80, Profesa Maathai alikamatwa, kupigwa na kuteswa wakati wa utawala wa Rais Moi baada ya kupinga sera zilizosababisha uharibifu wa mazingira. Mwaka 2002 alichaguliwa kuwa mbunge na mwaka 2003.

Pia, Profesa Wangari  aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mazingira nchini Kenya wakati wa utawala wa Rais Mwai Kibaki, Januari 2003 hadi Novemba 2005.

Wangari ambaye ni Profesa wa maumbile ya wanyama wakati akipokea tuzo yake, alisema kilichompa nguvu katika harakati zake ilikuwa ni kumbukumbu ya utoto wake wakati miti ilipokuwa inakatwa kiholela na kusababisha ukosefu wa kuni, maji masafi, chakula na mapato.

Kazi hiyo ilimfanya akapewa tuzo ya amani akiwa mwanamke Mkenya wa kwanza, Mwafrika wa kwanza na mwanaharakati wa kwanza wa mazingira kupata tuzo hiyo.

Pia, Profesa Wangari  alianzisha vuguvugu la Green Belt mwaka 1977, utaratibu uliosababisha miti kati ya milioni 20 hadi 30 kupandwa duniani.

Mradi huo ulianzishwa kwa lengo la kutunza mazingira na ulitoa fursa ya kutetea haki za wanawake.

Alisema wanawake walijiunga na mradi huo na kutambua kuwa mabadiliko yanafaa kutekelezwa katika nyanja kubwa zaidi.

Profesa Wangari alifariki dunia mwaka 2011 kwa ugonjwa wa kansa.

No comments