Breaking News

UPASUAJI MKUBWA WA KUPANDIKIZA USO WAFANYIKA UFARANSA

Jérôme Hamon aliishi miezi miwili bila uso Ufaransa

NA MWANDISHI WETU
Mtu wa kwanza duniani kupandikizwa nyuso mbili amesema kuwa anahisi vyema miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji huo.
Uso wa kwanza wa Jerome Hamon ulitolewa mwaka uliopita baada ya kupata ishara za kukataliwa kufuatia matibabu ya dawa ya antibiotic wakati aliposhikwa na homa.
mtu aliyefanyiwa upasuaji wa uso ufaransa
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 43 alisalia hospitalini mjini Paris bila uso kwa miezi miwili huku mfadhili wake akitafutwa.
Alisema: Uso wake wa kwanza aliukubali mara moja .Bwana Hamone anaugua ugonjwa unaosababisha uvimbe katika uso.
Upandikizaji wake wa kwanza 2010 ulifanikiwa , lakini akaambukizwa homa 2015 na kupewa dawa za antibiotics.
Dawa hiyo haikuingiliana na matibabu yake hatua iliosababisha damu yake kuukataa uso huo.
Ishara za kwanza za uso huo kukataliwa na damu zilianza kufichuka 2016 na Novemba iliopita. Ilibidi uso huo kuondolewa.
Bwana Hamon aliishi bila uso katia chumba kimoja katika hospitali ya Groges-Pompidou mjini Paris bila kuwa na uwezo wa kuona ,kuzungumza ama hata kusikia hadi mwezi Januari wakati ambapo mfadhili wa uso wake alipatikana na upandikizaji wa pili kufanywa.
Ili kuzuia uso huo kukataliwa na damu yake, bwana hamon aliyepewa jina Mtu mwenye 'nyuso tatu' na vyombo vya habari vya Ufaransa alipatiwa matibabu maalum kusaficha damu kabla ya upasuaji huo kufanyika.
Uso wake wa tatu ni mzuri ijapokuwa fuvu lake la kichwa , ngozi na vipengee vyake havijaingiliana vyema. lakini anaamini kwamba atapona.
''Iwapo ningekataa uso huu mpya ingekuwa vibaya sana . Ni Swala la utambulizi, lakini sasa tumefanikiwa ni vyema kwangu'', aliambia chombo cha habari cha AFP kutoka hospitali ambapo anaendelea kujiuguza.
Tangu wakati huo, takriban operesheni 40 za upasuaji zimefanyika kote duniani.

No comments