Breaking News

UWEZO MDOGO KIUCHUMI UNAATHIRI UZAZINA MWANDISHI WETU

UPO uhusiano mkubwa kati ya umasikini, kiwango cha elimu na suala la uchumi.
Katika jamii suala la kuwepo watu wa aina tofauti haliwezi kukwepeka.

Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia hali halisi, kujitathmini na kuchagua aina ya maisha tunayoyataka.
Wastani wa idadi ya watu katika kaya moja nchini ni watu watano, huku kaya moja kati ya 10 zikiongozwa na wanawake.

Asilimia 46 ya watu wote katika kaya ni watoto walio chini ya umri wa miaka 15.
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti wa mpango wa kimataifa wa DHS, ambao husaidfia nchi mbalimbali katika ukusanyaji wa taarifa muhimu kwa ajili ya kutathmini na kufuatilia sekta mbalimbali ikiwemo afya, lishe na idadi ya watu.

UMILIKI MALI
Takwimu za DHS zinaonyesha suala la umiliki mali kwa Watanzania kwamba hivi sasa, kati ya kaya tatu hadi nne zinamiliki simu za mkononi.

Asilimia 50 ya kaya zote zinamiliki redio ambapo kaya nne kati ya 10 zinahodhi baiskeli, sawa na asilimia 40 ya Watanzania.

Asilimia 20 ya kaya zote nchini zinamiliki luninga na kaya zinazomiliki angalau gari moja ni asilimia nne.

Utafiti huo unaonyesha kwa kaya za mijini kwa  Tanzania Bara, zinao uwezo wa kumiliki mali hizo kuliko kaya maeneo ya vijijini.

Hata hivyo, kaya za vijijini kwa Tanzansia Bara, zinao uwezo mkubwa wa kumiliki raslimali, hususan ardhi, kwa ajili ya kilimo na ufugaji kuliko kaya za mijini.

Kwa upande wa Zanzibar, takwimu hiizozinaonyesha kwamba kaya zinamiliki mali kwa kiwango kikubwa.

Asilimia 93 ya idadi ya watu wanamiliki simu za mkononi, redio asilimia 62, baiskeli silimia 52  na wanaomiliki raslimali ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji ni asilimia 29.

MAJI, USAFI NA UMEME

Takwimu hizo zinaonyesha kwamba kaya sita kati ya 10 sawa na asilimia 61, zinapata maji kutoka katika vyanzo vilivyoboreshwa, ambavyo si vya kuchangia na kaya zingine.

Katika kaya za mijini Tanzania Bara, asilimia 86 wanapata maji kutoka katika vyanzo vilivyoboreshwa ikilinganishwa na asilimia 48 ya kaya vijijini.

Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, idadi ya kaya zinazopata maji kutoka katika vyanzo vilivyoboreshwa ni sawa na asilimia 98.

Pia matokeo ya utafiti yanaonyesha, miongoni mwa kaya nne kati ya 10 kote nchini, zinatumia dakika 30 au zaidi kupata maji ya kunywa.

Takribani kaya mbili kati ya 10 sawa na asilimia 19, zinatumia vyoo vilivyoboreshwa, ambavyo si vya kuchangia na kaya zingine.

Tanzania Bara maeneo ya vijijini, asilimia 86 ya kaya zina vyoo duni, huku kwa upande wa mijini, asilimia 23 tu ya kaya ndizo zenye vyoo vilivyoboreshwa.

Kwa upande wa Zanzibar, vyoo vilivyoboreshwa ambavyo si vya kuchangia ni asilimia 59, ambapo asilimia 17 ya kaya Zanzibar hazina kabisa vyoo, idadi ambayo ni kubwa nchini.

Kwa upande wa nishati, takwimu hizo zinaonyeha kaya moja kati aya nne nchini, zinao umeme.
Suala la elimu haliwezi kutenganishwa na maendeleo ambapo takeimu hizo zinaonyesha asilimia 15 ya wanawake na asilimia nane ya idadi ya watu wote nchini, hawana elimu.

Idadi hiyo ya watu ni wale wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49, ambapo nusu ya wanawake na wanaume, wamemaliza angalau elimu ya msingi.

Asilimia 23 ya wanawake na 28 ya wanaume, wana elimu ya sekondari au zaidi.
Hata hivyo, asilimia 77 ya wanawake na 83 ya wanaume wa umri kati ya miaka 15 hadi 49, wanajua kusoma na kuandika.

Kuhusu hali halisi ya suala la uzazi hivi sasa nchini, wanawake wanazaa wastani wa watoto watano.
Takwimu hizo zinaonyesha kwa mwaka 2015 hadi mwaka jana, wastani huo umepungua ikilinganishwa na mwaka 1991 na 1992, kutoka watoto sita na kuendelea.

Hata hivyo, takwimu hizo zinaonyesha kuwa uwezo wa uzazi unatofautina kulingana na makazi na kanda, ambapo Tanzania Bara wanawake wanaoishi vijijini wanazaa wastani wa watoto sita na mijini watoto watatu hadi wanne.

Kwa upande wa Zanzibar, kwa jumla wanawake wanazaa wastani wa watoto watano.
Pia uwezo wa uchumi na viwango vya elimu, unachangia kwa kiasi kikubwa suala la uzazi.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, wanaawake wasio na elimu wanazaa wastani wa watoto watatu zaidi ya wanawake wenye elimu kuanzia ya sekondari na zaidi. Uwiano ni kati watoto watatu ana sita.

Hivyo, matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kwamba uwezo wa kuzaa unapungua kutokana na kiwango cha utajiri ikiwemo elimu katika kaya husika.

Wanawake wanaoishi katika kaya fukara wanazaa wastani wa watoto saba ikilinganishwa na wanaoishi katika kaya tajiri ambao wanazaa watoto watatu.

KUJAMIIANA

Takwimu hizo za DHS zinaonyesha kwamba wanawake wa Tanzania huanza kujamiiana mwaka mmoja mapema zaidi ya wanaume.

Wanawake huanza kujamiiana miaka katika wumri wa miaka 17 na wanaume miaka 18.
Pia wanawake wenye elimu ya sekondari au zaidi, huanza kujamiiana miaka mitatu zaidi ya wasio na elimu.

Asilimia 61 ya wanawake na 47 ya wanaume huanza kujamiiana katika umri usiozidi miaka 18.
Wanawake kutoka kaya tajiri huolewa miaka mitatu baada ya kuanza kujamiiana, ikilinganishwa na wanaotoka kaya maskini ambao huanza kujamiiana miaka miwili toka kuanza kufanya tendo hilo.

NDOA ZA MITALA

Matokeo ya utafiti huo yanaonyesha asilimia 18 ya wanawake Tanzania wapo katika ndoa za mitala, kwa kuwa na mke mwenza angalau mmoja.

Pia silimia 13 ya wanaume wanaotoka katika kaya zilizokithiri kwa umasikini wanaoa wanawake mitala.


Utafiti huo unaonyesha kwamba ndoa za mitala zipo nyingi zaidi kwa wanawake waio na elimu kwa asilimia 31, masikini 29 zaidi ya wenye elimu na wanaotoka katika kaya tajiri.

Hivyo takwimu hizi ni muhimu watanzania kuzingatia, ili kujua udhaifu ulipo na kujirekebisha.
Suala hili litasaidia kujikomboa kiuchumi na kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kaya, jamii na taifa kwa jumla.

No comments