Breaking News

HABARI KATIKA PICHA: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIVYOZINDUA MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUFUA UMEME KWA GESI ASLIA MTWARA JANA, MKOANI MTWARA

 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo litakalotumika kupakuwa mafuta kutoka kwenye Meli hadi kwenye matangi ya kuhifadhi mafuta katika Bandari ya Mtwara jana.Wapili kulia ni  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Tanzania, Deusdediti Kakoko.
 MAJENERETA mawili ya kuzalisha umeme yaliyonunuliwa na Serikali na kufungwa kwenye eneo la TANESCO lenye mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi asilia katika Manispaa ya Mtwara ili kupanua uzalishaji umeme wa gesi asilia Mtwara . Majenereta hayo yalizinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
 MAJALIWA akikata utepe wakati alipozindua Mradi wa Upanuzi wa Kituo cha Kufua Umeme kwa Gesi Asilia Mtwara jana. Watatu kulia ni  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditie , wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Gelasius  Byakanwa na kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah. (Picha zote na na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAJALIWA akifurahia jambo baada ya kuzindua Mradi wa Upanuzi wa Kituo cha Kufua Umeme kwa Gesi Asilia Mtwara.Watatu kulia ni Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atshasta  Nditie, wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa na kulia ni Mbunge  wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mradi wa Upanuzi wa Kituo cha Kufua Umeme kwa Gesi Asilia Mtwara.Wapili kulia ni Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa.

No comments