Breaking News

HABARI NJEMA KWA WANA UBUNGO, YAWA MIONGONI MWA HALMASHAURI BORA 17 TANZANIA

Hayo yamesemwa Leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Selikali za Mitaa,Mh.Suleiman Jaffo akitoa Neno la Shukrani Baada ya Meya na Mkurugenzi Ubungo pamoja na Halmashauri zingine kusaini Makubaliano ya Kupokea Fedha kutoka Wizara ya Fedha Mjini Dodoma.

Ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Imepokea Kiasi cha   Tsh Billioni 1 kutoka Wizara ya fedha.Na Kuwa Miongoni Mwa Halmashauri 17  zilizofanya Vizuri na Kufanikiwa kupitishiwa fedha hizo kwa kukidhi Vigezo baada ya Ushindani wa  kuandaa andilo la mradi  kwa kuzingatia fursa za Halmashauri,ambapo Halamshauri zote 185 zilishindanishwa.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Imeandika Mradi Ufufuaji wa Mradi  mkakati wa Soko Kubwa la Kisasa katika Soko la Mburahati,Ambapo Ujenzi huo wa Mradi ukipatiwa fedha utasababisha Manispaa ya Ubungo kujitegemea kujiendesha bila kutegemea ruzukuvya serikali kuu ifikapo 2025.pamoja na kuwa Chanzo kikuu cha Mapato na Ajira kwa Watu wa  Manispaa ya Ubungo.

Pichani ni Meya Boniface Jacob na Mkurugenzi wakisaini  Mkataba wa  makubaliano na Katibu Mkuu wizara ya fedha Ndugu Dotto James juu ya  kupokea fedha na kuanza Mradi huo kati ya Manispaa na Wizara ya fedha.

No comments