HATIMAYE KAMPUNI YA KUCHIMBA MADINI YA TANZANITE ONE YAKILI KOSA, YAKUBALI KUILIPA TANZANIA FIDIA, KODI. YAMMWAGIA SIFA JPM. NI BAADA YA KUUNDA TUME. SERIKALI YAAHIDI KUIPA USHIRIKIANO.
ANARIPOTI MWANDISHI WETU HATIMAYE Kampuni ya kuchimba madiniya
Tanzanite One imekubali kuilipa Serikali fidia pamoja na kodi watakayo kubaliana
kutokana na dosari zilizokuwepo hapo awali, imeelezwa.
Makubaliano hayo ya metiwasain
leo iJijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais, Dk. John Magufuli,
Profesa Palamagamba Kabudi na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma.
Akizungumza mara baada ya kutia
saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wakamati ya majadiliano kwa upande wa Serikali,
Profesa. Kabudi amesema Tanzanite One imekubali kulipa Serikali fidia kutokanana
na mambo iliyofanya ambayo yalikuwa kinyume na utaratibu ulioipa Serikali
hasara.
Alisema fidia hiyo inatakiwa
kulipwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza italipwa ndani ya wiki mbili kuanzia leo
na haitahusisha kodi.
Pia, Kampuni hiyo ya Tanzanite
One italazimika kulipa kodi kama kawaida inazodaiwa na Serikali na tozo nyingine
zote zinazo daiwa na Serikali.
Kwa mujibu wa Kabudi, Serikali
imekubaliana na Kampuni ya Tanzanite One kuwa itafuata masharti yote ya sheria ya
madini ya mwaka 2010 ambayo inaeleza kuwa ni Watanzania tu ndiowanaoruhusiwa kuchimba
madini ya Vito na endapo hawakutakuwa na uwezo, ndipo wanapoweza kuingia ubiana
wageni.
Aidha,Prof. Kabudi alisema, kuhusu
wachimbaji wadogo wadogo wa Tanzanite katika eneo la Mirerani, utaratibu mpya unawekwa
lengo kubwa likiwa ni kutekeleza sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inalenga
madini ya vito kuwa mikononi mwa Watanzania.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa
Kampuniya Tanzanite One Faisal Juma, alimshukuru Rais Magufuli kwa kuunda kamati
hiyo ya Kizalendo katika kufuatilia rasilimali za madini nchini ambapo wameweza
kujadiliana na kufikia muafaka wa kulipa fidia ikiwa ni mbali na malipo yote yaliyotakiwa
kulipwa Serikali ikiwemo kodi.
Alisema, Tanzanite One
itahakikisha inafuata taratibu zote za sheria ya madini ya mwaka 2010 kwa lengo
la kuhakikisha rasilimali ya madini inawanufaisha Watanzania na kwamba uvunjifu
wa sheria uliofanywa na kampuni hiyo hautajirudiatena.
"Sisi kama Tanzanite
One tunaihakikishia Serikali kuwa uaminifu uliotuonyesha nasi si pia kama Kampuni
tutahakikisha tunakuwa waaminifu na kuwa zao hil ilinanufaisha taifa kutokana na
imani aliyotuonyesha Rais kama wananchi wake kutupa nafasi na fursa ya kusikilizwa
ili kurekebisha makosa tuliyoyatenda", amesema Faisal.
Faisal alisema Tanzanite One
itahakikisha haitafanya makosa iliyofanya maraya kwanza na hivyo kuwa mfano wa kampuni
nyingine za madini kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania.
No comments