Breaking News

RAIS MNANGAGWA AIMWAGIA SIFA TANZANIA

MNANGAGWA AIMWAGIA SIFA TANZANIA NA Victoria Falls, Zimbabwe RAIS wa Zimbabwe, Emmerson Dambudzo Mnangagwa (mwenye skafu) akiwa na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) wa CCM, Kanali mstaafu, Ngemela Eslom Lubinga (mwenye miwani) pamoja na Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe (Mbunge) akiteta jambo na Rais Mnangagwa. Wengine katika picha ni washiriki wa Mkutano Mkuu wa Zimbabwe Center for Democracy (ZCD) uliomalizika leo katika Hotel ya Elephant Hills, Victoria Falls leo. Rais Mnangagwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa ZANU-PF, alihudhuria mkutano huo na alitoa shukrani nyingi kwa ujumbe wa Tanzania kwa kuwapa elimu na uzoefu mzuri utakaowasaidia kufanya uchaguzi wa kidemokrasia kwa amani na utulivu. Ujumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ulijumuisha vyama vitatu vya siasa vya CCM, NCCR MAGEUZI na ACT Wazalendo. Mnangagwa ni Rais wa pili wa Zimbabwe tangu ipate uhuru mwaka1980 kutoka kwa utawala wa walowezi. Wazimbabwe wanatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka huu ambapo Rais Mnangagwa atagombea tena.

No comments