Breaking News

WAZIRI MKUCHIKA AISHUKURU SERIKALI YA USWISS KWA USHIRIKIANO WAKE NA TANZANIA KATIKA SEKTA MBALIMBALI IKIWEMO MASUALA YA UTAWALA BORA.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu), George Mkuchika (Mb) akipokea zawadi toka kwa Balozi wa Uswiss nchini Tanzania na Zambia, Florence Tinguely Mattli aliyefika ofisini kwake Jijini Dodoma kujitambulisha.


BALOZI wa Uswiss nchini Tanzania na Zambia, Florence Tinguely Mattli akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (mstaafu), George Mkuchika  (hayupo pichani).


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (mstaafu), George Mkuchika (Mb) ameishukuru Serikali ya Uswiss kwa ushirikiano wake katika sekta mbalimbali ikiwamo masuala ya utawala bora.
Mkuchika aliyasema hayo leo katika kikao na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania na Zambia, Mhe. Florence Tinguely Mattli kilichofanyika ofisini kwake Jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa Mkuchika, Serikali ya Uswiss imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa kwa Tanzania katika masuala ya Utawala Bora ambayo wafadhili wengi hawayapi kipaumbele.
 Alizitaja nchi nyingine zinazoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya utawala bora kuwa ni Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la DfID na Marekani kupitia Shirika lake la Misaada la USAID.
 Aidha, Mkuchika alisema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wake, Dk. John Pombe Magufuli inahakikisha suala la utawala bora linazingatiwa katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
Kwa upande wake Balozi wa Uswiss nchini Tanzania na Zambia, Florence Tinguely Mattli aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada wanazozifanya katika utekelezaji wa masuala ya utawala bora na ameahidi kuendeleza ushirikiano.

No comments