Breaking News

WAZIRI MKUU MAJALIWA: TANZANIA BADO INAHITAJI WAWEKEZAJI. AMTAKA BALOZI KIDATA KUTUMIA VIZURI FURSA YA UWEPO WAKE NCHINI KANADA KWA MANUFAA YA WATANZANIA
 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia),  akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Alphayo Kidata, ambaye alikwenda  nyumbani kwake Majaliwa,  Oysterbay  Jijini Dar es Salaam  jana, kumuaga. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 WAZIRI MAJALIWA: TANZANIA BADO INAHITAJI WAWEKEZAJI. AMTAKA BALOZI KIDATA KUTUMIA VIZURI FURSA YA UWEPO WAKE NCHINI KANADA KWA MANUFAA YA WATANZANIA.
NA MWANDISHI MAALUMU.
WAZIRI MKUU KaWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Alphayo Kidata ambaye alikwenda  kwenye Makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay  jijini Dar es salaam kuaga, Mei 23, 2018.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkssim Majaliwa amesema Tanzania bado inahitaji wawekezaji na kupitia kwenye uwekezaji, inapata fursa ya mitaji na teknolojia za kisasa.
 Ayasema hayo jana Jijini Dar es Salaam,  wakati akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Alfayo Kidata ambaye alikwenda kumuaga nyumbani kwake.
 Waziri Mkuu alimtaka Balozi Kidata atumie fursa ya uwepo wake nchini Canada kuangalia namna ya kuisadia nchi kuiimarisha katika sekta ya kilimo, madini na utalii.
 “Tukiimarisha sekta hizi, uchumi ndani ya nchi unakua, lakini pia tunategemea kutumia nchi rafiki kukuza uchumi wetu wa ndani kwa maana ya kukuza mitaji na kupata teknolojia za kisasa,” alisema.
mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano, lakini zaidi mkakati wetu wa kukuza uchumi wa viwanda,” alisisitiza Waziri Mkuu.
 Pia, alimtaka Kidata kusimamia suala la upatikanaji wa masoko kwa ajili ya mazao yanayozalishwa nchini ili wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi.
 “Hapa nyumbani tuna mazao matano ambayo tumeazimia kuyafufua lakini masoko ya ndani hayatoshi, kwa hiyo kazi yako mojawapo ukiwa huko ni kututafutia masoko,” amesema.
 Waziri Mkuu alimweleza Balozi Kidata azingatie pia suala zima la kuongeza idadi ya watalii. “Tunataka ukasaidie kutangaza nchi yetu ili watalii waje kuona vivutio vyetu. Tunataka kuongeza idadi ya watalii kutoka milioni mbili ya sasa hadi kufikia milioni tano ifikapo mwaka 2020,” alisema Majaliwa.
 Aidha Waziri Mkuu alimtaka Kidata akiwa huko afuatiilie  fursa za masomo kwa ajili ya Watanzania wanaotaka kusoma Canada na Cuba. “Nilipoongea na Makamu wa Rais wa Cuba, aliahidi kuongeza idadi ya Watanzania wanaotaka kusomea udaktari. Kwa hiyo, ukifika itabidi ufuatilie ahadi hiyo,” aliongeza kusema Waziri Mkuu.
 Katika hatua nyingine, Majaliwa alimsisitizia Balozi Kidata akifika Canada, awatambue na kuwaunganisha Watanzania waishio nchini humo na awahamasishe wafanye kazi ili waweze kuwekeza nyumbani.
 Kwa upande wake, akizungumza baada ya kuagana na Waziri Mkuu, Balozi Kidata alisema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa na Waziri Mkuu.
 Alisema anatambua kwamba Canada ina idadi ya watu zaidi ya milioni 40 na atafanya juhudi zaidi za kuitangaza Tanzania ili waje kuona vivutio vilivyopo nchini. Pia atafuatilia fursa za mafunzo kwa wanafunzi wa Kitanzania.
 “Kwenye suala la uchumi wa viwanda, tunahitaji kuwa na uzalishaji wa mazao ya kutosha. Kwa hiyo tunahitaji kuwana kilimo cha uhakika na cha muda wote kuliko. Tunahitaji kupata utaalamu na mitaji kwa ajili ya mashamba ya umwagiliaji,” alisema.
 Alisema kuwepo kwa kilimo cha umwagiliaji, kutasaidia kuwe na uhakika wa upatikanaji wa malighafi zitazakotumika kwenye viwanda.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Alphayo Kidata.
MAJALIWA na Kidata wakifurahia jambo.
WAZIRI Mkuu Majaliwa na Balozi Kidata wakiagana baada ya mazungumzo yao.

No comments