Breaking News

MBAO FC WANOGESHA K/KOO DERBYNa John Richard.
WALANDA mbao wa mkoa wa Mwanza Mbao Fc wamerejea kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara (TPL) mara baada ya kuwashikisha adabu wajelajela Tanzania Prison kwa bao 1-0, katika mchezo uliomalizikia hii leo.

Huu ni ushindi wa pili mfululizo ambao klabu hiyo yenye maskani yake jijini Mwanza  hasa  katika uwanja wao wa nyumbani mara baaada ya kutoka kuwanyoa mabingwa waetetezi wikiendi iliyopita kwa bao 1-0.


Alikuwa ni ndaki Robert aliyewaweka Mbao kileleni kunako dakika ya 90 ya mchezo kwa kupachika bao na Mbao kuibuka kidedea.
Matokeo hayo yanaifanya Mbao kulejea kileleni wakiwa na pointi 13 mara baada ya kucheza michezo sita wakifatiwa na Yanga Sc, wenye pointi 12 kwa michezo minne waliyoshuka dimbani.

Azam wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 11, na nafasi ya Nne ikikaliwa na mabingwa watetezi Simba wenye poin
Mchezo mwingine ulipigwa katika dimba la Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara, wababe wa Mtibewa Sugar na Simba Sc Ndanda Fc wanakuchele kupokea kipigo cha mabao 1-3 kutoka kwa Stand United.

Ndanda waliingi kwenye mchezo huo wakiwa wanajiamini baada ya kuwachapa Mtibwa Suigar kwa mabao 2-1, na kwenda suluhu na Simba.
Shughuli nyingine ilikuwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa African Lyon kupokea kichapo cha mabao 0-2 dhidi ya wakata miwa wa Manungu Mtimbwa Sugar.

Mtibwa walikuwa na kiu kupata pointi tatu mara baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Ndanda Fc, mchezo wa mwisho kabla ya kukutana na African Lyon.

Kwa ushindi huo mtibwa wanafikisha pointi 10 na kuwa nyuma ya Simba kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakiwa nafasi ya 5.
Mwisho.

No comments