Breaking News

MASAUNI ‘SERIKALI IMEJIPANGA KUTOKOMEZA UHARIFU’Na Mwandishi Wetu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali imeweka mpango mkakati wa kuhakikisha uharifu unatokomea katika maeneo ya kitali.

Mhandisi Masauni amesema kuwa mpango uliopo ni kutumia vituo vya polisi vinavyo hamishika maarufu kama mobile police post ambavyo amesema vimeanza tayari kutumika.

Hata hivyo Mh. Naibu Waziri amewataka  wadau wa sekta ya utalii kujitolea ili kuipa nguvu sekta hiyo iweze kupambana na uhalifu unajitokeza mara kwa mara.

“kama wadau wa sekta ya utalii wanaweza kushirikiana na sisi kuchangia, tunaweze kuwatumia askari wetu jamii ili kutusaidia kuthibiti matatizo ya kiharifu yanayo jitokeza”.
No comments