Breaking News

SIMBA KAMA ANA NAWA TAIFA.Na John Richard.
MNAYAMA kala nyama ya mtoto, ndivyo unaweza kusema baada ya kumalizika kwa mtanange wa Ligi kuu Tanzania bara.(TPL) Simba SC dhidi ya Alliance Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku mchezo huo ukimpa faida mwenyeji Simba sc kuibuka na ushindi wa magoli 5-1.


Mabao ya Simba yamewekwa kimiani na Emmanuel Okwi mawili, Chama, Salamba na aliye Kwasi aliyeanza leo akichukua namba ya nahodha Mohamed Hussein.


Kipigo hicho ni cha pili mfurulizo kutoka kwa wakongwe hao TPL kuwashushia Alliance mara baada ya Wikiendi iliyopita vijana wa  Mbwana Makata wenye maskani yao Jijini Mwanza  kulala 3-0 mbele ya Wanajangwani mabingwa wa kihistoria Yanga.

Simba wamepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 20 nyuma ya vinara Azam wenye pointi 24.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo kadhaa kupigwa wakati mechi inayosubiliwa kwa hamu ni ule wa KMC vijana wa mjini watakapowaalika Yanga Uwanja wa Taifa.

No comments