Breaking News

STARS KULA BATA NA RAISNa Mwandishi Wetu.
Wachezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania kwa pamoja leo hii watapata fulsa ya kula chakula cha mchana pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais amewaalika wachezaji hao mkufuatia kuibuka kwa matuamaini mapya ya kufudhu kuelekea katika ya michuano ya mataifa ya Afrika itakayo fanyika nchini Cameroon ambapo Taifa Stars iliibuka na ushindi wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Cape Verde na kuwawezesha kusogea mpaka nafasi ya pili wakiwa na alama tano nyuma ya Uganda wenye alama 10.


Hii ni kwa ajili ya kutoa motisha na pongezi kwa wachezaji wa Taifa Stars ambao wanalipambania Taifa kuelekea katika michuano mikubwa  barani Afrika.

Stars imebakiza michezo miwili mmoja ugenini dhidi ya Lesotho na ule wa nyumbani dhidi ya Uganda na kama wataibuka na matokeo mazuri basi watatinga Afcon kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kujaribu bila mafanikio.

No comments