VIJANA WATAKIWA KUGEUKIA KILIMO ILI KUJIKWAMUA DHIDI YA UMASIKI
Na Mwandishi Wetu.
Makamu wa pili wa
Rais wa ZanZibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka vijana kote nchini kuachana na
kasumba ya kusubiri serikali iwaajili na kauamua kugeukia kilimo kwakua ni moja
kati ya biashara zinazolipa kwa sasa duiani.
Balozi Seif Ali
Iddi alisema hayo wakati akiyafunga Maonyesho ya Kilimo katika kuadhimisha Siku
ya Chakula Duniani yaliyofanyika katika Kijiji cha Chamanangwe Wilaya ya Wete
Kisiwani Pemba ambapo Makundi ya Wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Pemba
walipata fursa ya kuyatembelea na kujifunza mbinu tofauti za Kilimo.
Aliseama wakati
umefika kwa vijana kutambuawa kuwa kilimo ni biashara kubwa duniani kwa
sasa kama biashara nyingine na kama vijana watageukia katika biashara
hiyo basi wataondokana umasikini.
Aidha alisema
amefurahishwa sana na muitikio wa wananchi wengi walio jitokeza katika
maonyesho hayo.
“ Nimefarajika
Kuona Wananchi na Wakulima wa Mikoa Miwili ya Pemba jinsi walivyojitokeza
kutembelea Maonyesho haya yaliyofanyia kwa mara ya kwanza kisiwani Pemba.”
Katika hatua
nyingine Balozi Seif Ali Iddi aliutaka uongozi wa wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo
na Uvuvi kuchukua jitiahada za makusudi
katika kuhakikisha wanapandikiza elimu hiyo kwa kwa vijana ili kuwawezesha
vijana kote inchini waweze kutokana na kasumba ya kupenda kuajiliwa na
serikialai ambayo haina ofisi za kutosha kumwajili kila mtu.
Hata hivyo makamu
wa pili wa Rais alisema serikali inatambua kuwa wakulima na wafugaji
wengi nchini wanakabiliwa na kipato kidogo kinacho hitaji kupewa msukumo hivyo
akaziomba sekta binafsi nchini pamoja na zile za kimataifa kutoa mokopo nafuu
kwa wakulima na wafugaji wadogo wa dogo ili kuongeza uzalishaji nchini
picha zote kwa msaada wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
No comments