Breaking News

DKT. NDUGULILE ASIKITISHWA NA HUDUMA DUNI ZA MATIBABU ZINAZOTOLEWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA BOMBO *ATAKA ONGEZEKO LA MAPATO LIENDE SAMBAMBA NA UBORA WA HUDUMA.NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile, akizungumza na wagonjwa waliofika Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa ya Bombo, leo..
Na.WAMJW, Tanga

 UONGOZI  wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bombo, umetakiwa  kuboresha huduma za matibabu zitakazopatikana na kwa muda mfupi ili kupunguza adha ya wagonjwa kukaa muda mrefu. 

Hayo yalisemwa leo Novemba 27, 2018 na  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndungulile, wakati wa ziara yake hospitaliji hapo.

Katika ziara hiyo, Dk. Ndugulile alibaini uwepo wa idadi  kubwa ya wagonjwa wanaosubiri huduma huku kasi ya madaktari wanaotoa huduma hiyo kwa wagonjwa ikiwa ni ndogo, hivyo kuleta  usumbufu mkubwa  kwa wanaofika hospitalini hapo kutokana na kutumia muda mwingi kusubiri huduma.                         DK. Ndungulile akikagua nyaraka mbalimbali hospitalini hapo


 "Nimeona  f ursa ya hospitali hii kukusanya mapato  zaidi ya hapa hivyo, mnatakiwa kuboresha huduma za matibabu kwa kuweka mfumo wa serikali wa kukusanya mapato kwa kuunganisha idara zote za hospitali hii,” alisema Dk.Ndugulile.

Aliongeza kuwa huduma ya hospitali hiyo bado sio nzuri kwani ameona hawana utaratibu mzuri kwa kuwa wagonjwa wanafika  toka sa./////,,,mmnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnna 12 ]';nxasubuhi lakini hadi mchana bado hawajapata matibabu.

"Bado hakuna utaratibu mzuri wa kuwaona wagonjwa,haijulikani yupi aliyewahi, yupi amechelewa, ninawaagiza muweke utaratibu mzuri utakaowawezesha wagonjwa kupata huduma ndani ya muda mfupi na wazee wapatiwe kipaumbele,” alisema Dk.Ndugulile. Dk. Faustine Ndugulile (wa pili kulia), akipata maelezo toka kwa Mganga Mfawidhi wa  Hospitali ya Bombo Dk. Jumanne Ngaiwa (kushoto), kuhusu ujenzi wa jengo la matibabu ya dharura.Aidha,Naibu Waziri huyo aliwataka watumishi wote hospitaliji hapo kuweka kumbukumbu za  nyaraka za wagonjwa  vizuri kwa kuandika tarehe na muda wanaowahudumia wagonjwa wao.

"Umemwita daftari hajafika andika kwenye jarada ili baadae tukija tubaini  kama  mgonjwa amecheleweshwa kupata huduma ni wapi watendaji w etu walizembea"alisema Dkt.Ndugulile.

NAIBU Waziri Dk. Faustine Ndugulile akipokea maelezo ya namna ya upatikanaji wa huduma kwa mtumishi wa afya katika Hospitali ya Bombo.


Hata hivyo,  wakati wa ziara hiyo  Naibu Waziri Ndungulile, alibaini jengo la wagonjwa mahututi limekamilika lakini halina  madaktari wenye sifa kutoa huduma kwa wagonjwa hao  na hivyo,  kuwataka watendaji wa wizara yake kushughulikia  haraka suala hilo.

                                      DK. Ndungulile akitazama dawa za wagonjwa

Akiwasilisha taarifa ya hospitali  Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Jumanne Ngaiwa,  alisema  kuongezeka kwa mapato katika hospitali hiyo imetokana na upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kwa ujumla huku makusanyo kwa mwezi inakadiliwa kutumia milioni 69 kwa makusanyo ya papo kwa papo na mapato yanayotokana na mfumo wa bima ya afya ni milioni 239 hadi 300.

No comments