Breaking News

PAC: TUTAISHAURI SERIKALI IPELEKE FRDHA NYINGI KWA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA. *YASEMA IMERIDHISHWA NA MIRADI INAYOITEKELEZA.


BAADHI ya Wajumbe wa Kmati ya PAC na TAMISEMI wakiwa katika ziara ya kikazi jana


Zulfa Mfinanga, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema itaishauri serikali kupeleka fedha nyingi zaidi kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kuwa ndipo penye wananchi wengi na wenye kipato cha chini.

Akizungumza mara baada ya kutembelea vituo vya afya vya Bahi, Mndemu, Hombolo pamoja na Makole, Mwenyekiti  wa kamati hiyo Naghenjwa Kaboyoka ameipongeza serikali kwa kuwekeza kwenye huduma za afya ngazi ya chini na kwamba ni vema ikaendelendea kuiwezesha Wizara hiyo ili kila mwananchi aweze kupata huduma bora ya afya na kwa haraka.

“Naipongeza TAMISEMI imefanya mambo makubwa sana, naishauri serikali ipeleke fedha nyingi zaidi, huku ndipo penye wananchi wengi wenye kipato cha chini, na tunafahamu kuwa mtu mwenye kipato cha chini mara nyingi ndiye anayesumbuliwa na maradhi mbalimbali” Alisema Kaboyoka.

Kwa upande mwingine mwenyekiti huyo ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa ujenzi wa vituo hivyo ambavyo kila kimoja kilipewa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati ambapo ujenzi wa vituo hivyo umefikia zaidi ya asilimia 90 na kusema kazi iliyofanyika inatia moyo hivyo hana budi kumuunga mkono Rais John Pombe magufuli.“Ingawa bado sijakaa na kamati yangu kwa ajili ya kufanya tathmini ya fedha zilizotumika, lakini kwa muonekano tu wa macho tumeona kazi iyofanyika ni kubwa na inatia moyo, pongezi hizi ziende kwa Rais, Waziri Jafo pamoja na wote walioshiriki” Alisema Kaboyoga.

Akizungumza wakati ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt Zainab Chaula ameiambia kamati hiyo kuwa serikali imetoa fedha kwa ajili wa ujenzi wa vituo 350 nchini nzima na kwamba hadi kufikia mwaka 2020 vituo vyote 518 nchini vitakuwa vimeshafanyiwa ukarabati mkuwa.

Akiwa katika kituo cha afya Bahi ambacho hivi karibuni kitaanza kutoa huduma ya dharura pamoja na ya upasuaji tofauti na hapo awali, Dkt Chaula amesema kutokana na uimarishaji wa huduma za afya kwa sasa wananchi watapiga hatua kimaendeleo kwa kuwa afya njema ndiyo msingi wa maendeleo.

Naye mwenyekiti wa kamati ya TAMISEMI, Danson Rwekiza amesema ni hatua ya kujivunia kwa sasa kwani kwa mwaka mmoja serikali imeweza kujenga na kukarabati  vituo vya afya  350 tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa na vituo vya 380 vilivyojengwa tokea nchi ipate uhuru.


Kwa upande wao wananchi waliozungumza na kamati hiyo hususani akina mama waliojifungua waliokuwa wodini wameonyesha furaha baada ya kuboreshewa na kusogezewa huduma ya afya tofauti na hapo awali ambapo wengi wao walilazimika kujifungulia majumbani.

Leo kamati hiyo inaendelea na ziara ya kutembea vituo vya katika wilaya za Chamwino na Kongwa.

Juu pichani ni baadhi ya majengo ya miradi yaliyokaguliwa na kamati hizo

No comments