Breaking News

SEIRIKALI YA MISRI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NCHINI.


KATIBU Mkuu wa  Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabrie (kulia)l, akitoa maelezo kwa Kaimu Balozi wa Misri nchini, Nevine El-Saeed na Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi huo Mohamed Ibrahim, katika ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar es Salaam jana.

Na Edward Kondela

 KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Misri hapa nchini, Nevine El-Saeed, pamoja na kupokea andiko la awali la nia ya Serikali ya Misri kutaka kuwekeza nchini katika sekta ya mifugo.
Kaimu balozi huyo, ambaye aliambatana na Mkuu wa Idara ya Uchumi wake, Mohamed Ibrahim, katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo Jijini Dar es Salaam, alisema jana kuwa serikali ya nchi hiyo inahitaji kuwekeza hapa nchini ili kufungua fursa mbalimbali ambazo zitapatikana kupitia uwekezaji huo.
KATIBU  Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel, akiongoza kikao cha namna bora ya uwekezaji wa Serikali ya Msri katika sekta ya mifugo nchini. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Misri nchini, Nevine El-Saeed na Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi huo, Mohamed Ibrahim.


Akizungumza na maofisa hao pamoja na wajumbe waliohudhuria kikao hicho, Katibu Mkuu  Ole Gabriel, alisema Tanzania ina mifugo mingi na kwamba ikitumika vizuri kupitia uwekezaji, ambapo nia ya Serikali ya Awamu ya Tano imejikita zaidi kupitia kufufua na kuanzishwa kwa viwanda vipya kutaongeza fursa nyingi zaidi zikiwemo za ajira.
Aidha, alisema atahakikisha  anasimamia  ipasavyo nia ya Serikali ya Misri kufanikisha uwekezaji huo ambao alisema wizara yake itahakikisha inaweka mazingira yatakayofanya uwekezaji huo uwe endelevu na kuleta tija kwa nchi zote mbili.
KAIMU Balozi wa Misri nchini,  Nevine El-Saeed,  akisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani),  wakati akifafanua namna bora ya uwekezaji wenye tija kwa nchi zote mbili..


Kikao hicho pia kimehudhuriwa na wakuu wa idara zilizo chini ya ofisi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wawakilishi kutoka Dawati la Sekta Binafsi, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Kituo cha Kuendeleza kilimo Nyanda za juu Kusini (SAGCOT) na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.


KATIBU  Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel,  akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Misri nchini,  Nevine El-Saeed, Mkuu wa Idara ya Uchumi katika ubalozi huo,  Mohamed Ibrahim na wajumbe waliohudhuria kikao kujadili nia ya serikali ya Misri kuwekeza katika sekta ya mifugo. Kikao kimefanyika  jana katika ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

No comments