Breaking News

SERIKALI YAJADILI UWEKEZAJI BORA ZAIDI WA MISRI KATIKA SEKTA YA MIFUGO *WAZIRI MPINA ASEMA ANATAKA UWEKEZAJI WENYE KULETA TIJA KWA TAIFA.


WAZIRIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wakuu wa Idara zilizochini ya wizara yake na wadau wengine wa sekta ya mifugo, kujadili namna bora zaidi ya Serikali ya Misri kutaka kuwekeza katika sekta hiyo jana, Jijini De es Salaam.

Na Edward Kondela

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina, ameongoza kikao cha Wakuu wa Idara zilizo chini ya wizara yake pamoja na wadau wengine wa sekta yamifugo, kujadili namna bora zaidi ya Serikali ya Tanzania inavyoweza kunufaika na uwekezaji katika sekta ya mifugo kutokana na nia ya Serikali ya Misri kutaka kuwekeza katika sekta hiyo iliyoonyeshwa siku chache zilizopita.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar es Salaam jana, Waziri Mpina, aliwaambia wajumbe wa kikao hicho wakiwemo wawakilishi kutoka SUMA JKT, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Dawati la Sekta Binafsi, kuwa na mikakati ambayo itasaidia uwekezaji huo uwe na tija kwa taifa.
MMOJA wa wajumbe walioshiriki kikao hoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana, akiwakilisha hoja, wakwanza kushoto ni Waziri Mpina.

Aidha, Waziri Mpina alisema serikali inahitaji wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, lakini ni muhimu yakaandaliwa mazingira bora zaidi ili uwekezaji huo uwe endelevu na kuleta tija kwa taifa na wananchi kwa ujumla.


BAADHI ya wajumbe hao wakishiriki katika kikao hicho jana. Kulia ni Mpina.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho, wamemshauri Mpina masuala mbalimbali yakiwemo ya kitaalam pamoja na vifungu vya kisheria ili mikataba itakapoandaliwa na kusainiwa kati ya serikali ya Tanzania na Misri, iweze kuleta faida kwa nchi hizo mbili.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, akisoma baadhi ya mapendekezo yaliyoandaliwa na wajumbe wa kikao kuhusu uwekezaji katika sekta ya mifugo kutokana na nia ya Serikali ya Misri kutaka kuwekeza katika sekta hiyo.

Hivi karibuni Kaimu Balozi wa Misri nchini, Neville El-Saeed na Mkuu wa Kitengo cha Uchumi katika ubalozi huo, Mohamed Ibrahim, walifika katika ofisi ndogo za wizara hiyo katika siku tofauti ambapo walipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Luhaga Mpina, kuhusu uwekezaji huo.
    MPINA akisikiliza hoja za wajumbe hao.

Maofisa hao pia walikutana na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel na kumkabidhi andiko la awali la nia ya serikali ya nchi hiyo kutaka kuwekeza katika sekta yamifugo na kufungua fursa zaidi zilizopo katika sekta hiyo.

No comments