Breaking News

SERIKALI YAZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI *YATAKA WATAKAOPEWA KUFANYA SHUGHULI ZILIZOELEKEZWA KWENYE VIBALI VYAO.
 WAZIRI  Mkuu, Kassim Majaliwa,  akisalimiana na  Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Nchini, Dk. Anna Makalala, wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere Jijini Dar es salaam  kuzindua  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki leo Novemba 26, 2018.  Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dk. Augustine Mahiga  (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amezindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki na amewataka watu wote watakaopewa vibali hivyo kutii sheria kwa kufanya shughuli ambazo wameelekezwa kwa mujibu wa vibali vyao na si vinginevyo.

Alisema, utoaji wa huduma hizo ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kuvutia uwekezaji, hususan kwenye sekta ya viwanda kwani hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa vibali hivyo kwa raia wa kigeni na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi.

MAJALIWA, akisalimiana na Viongozi wa Idara ya Uhamiaji wakati alipowasili kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere.

Waziri Mkuu aliyasema hayo leo Novemba 26, 2028, wakati akizindua huduma hiyo  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo itasaidia kuondoa urasimu na ucheleweshwaji wa huduma pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.

Alisema kuwa Idara ya Uhamiaji inatarajia kuanza kutoa huduma tajwa kwa raia wa kigeni muda wowote kuanzia sasa na kwa kupitia huduma hiyo, raia wa kigeni wataweza kuomba vibali hivyo kwa njia ya kielektroniki wakati wowote na mahali popote walipo.


BAADHI  ya Washiriki wa uzinduzi wa  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani).  


Waziri Mkuu alisema watakaopewa vibali wanatakiwa kufanya shughuli zao kwa mujibu wa vibali vyao kwa sababu kufanya shughuli tofauti na ilivyoainishwa kwenye kibali ni kosa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uhamiaji.

Kwa mujibu wa Mjaliwa, matumizi ya mtandao katika utoaji wa huduma za viza na vibali vya ukaazi ni hatua ya mfano, kwani inakwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na sera ya Serikali ya matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Serikali (e-government).

                                                  BAADHI ya washiriki hao

Hata hivyo, Waziri Mkuu Majaliwa, alisema Serikali inatarajia kuwa, matumizi ya mifumo hiyo itaongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kwa kuwa mteja ataweza kulipia huduma hizo mwenyewe moja kwa moja pasipo kupitia kwa mawakala au mtu yeyote.

“Natoa wito kwa Maafisa, Askari pamoja na Watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji kuhakikisha kuwa mifumo hiyo inatunzwa pamoja na kuendeleza miundombinu yote ya kiutendaji,”alisisitiza Majaliwa. 

                                   WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia

Waziri Mkuu alisema kwa kuzingatia ahadi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na raia wa kigeni, Maofisa Uhamiaji wanatakiwa kutoa huduma hiyo kwa wakati, weledi na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Uhamiaji.


 NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi huo. MAJALIWA (kushoto),  akisalimiana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde baada ya kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere.


                                    MAHIGA akizungumza katika uzinduzi huo.


                                                   WAZIRI Mkuu Majaliwa akihutubia                                        KAMISHINA Jenerali Dk. Anna akihutubia


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dk. Augustine Mahiga,  kulia ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad  Masauni.


                                                       MHANDISI Masauni akihutubia.

Majaliwa alisema, mfumo wa huduma hizo utaunganishwa na mifumo mingine ya serikali, ambayo inatoa huduma kwa wananchi na wageni kama vile Mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Idara ya Kazi – Ofisi ya Waziri Mkuu, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mfumo wa Malipo ya Serikali Kimtandao (GePG). 

No comments