Breaking News

UBADHIRIFU WA ZAIDI SH. BILIONI TATU WILAYANI NYANGW’ALE WAMTIA KICHEFUCHEFU WAZIRI MKUU * AAGIZA WAHUSIKA WOTE WAKAMATWE NA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Sabasaba kilichopo Karumwa wilayani Nyang'hwale, jana Novemba 28, 2018. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
                                             Na Mwandishi Wetu, Geita
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameagiza watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyangw’ale waliohusika na ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni tatu fedha ambazo zilitolewa na Serikali kugharamia miradi ya maendeleo wachukuliwe hatua.
Pia ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa Mkaguzi wa Ndani wa halmashauri hiyo, Gavana Matesa, kwa sababu ameshindwa kutoa kwa mamlaka husika kuhusu taarifa za wizi wa fedha za maendeleo zilizotafunwa.
Waziri Mkuu alitoa agizo hayo jana Novemba 28, 2018 wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya hiyo  akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Geita.

 MAJALIWA, akizungumza na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi katika mkutano huo.

Miongoni mwa miradi ambayo fedha zake zimepotea ni pamoja na sh. bilioni 1.2 za ujenzi ofisi ya halmashauri hiyo, sh. milioni 400 za ukarabati wa kituo cha afya Nyangw’ale, sh. milioni 611.230 za miradi ya maji.
Nyingine ni sh. milioni 536.119 za mpango wa malipo kulingana na huduma (EP4R), sh. milioni 125.914 za ushuru wa huduma, sh. milioni 31 za ujenzi wa ofisi ya mbunge na sh. milioni 109 za mfuko wa barabara.
“Wilaya ya Nyangw’ale ni mpya na Serikali imekuwa ikileta fedha nyingi lakini fedha zote zimetafunwa, Serikali ipo makini sana na moja kati ya vita kubwa ni dhidi ya mafisadi, wala rushwa ambayo ni endelevu hivyo tutashughulika na kila mmoja,” alisema Majaliwa.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga aliyehamia CHADEMA, Hamis Mgeja ambaye alijumuika na  maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye Kiwanja cha  Sabasaba cha Karumwa wilayani Nyang'hwale.

Tayari watu saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyangw’ale, Carlos Gwamagobe, na wenzake wamekamatwa. Wizi unatisha Nyangw’ale wilaya inatia aibu tutawaondoa watu wote waliohusika na tutaendelea kuwakamata,” alisema.
Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali itahakikisha miradi yote iliyoahidiwa kujengwa kwenye wilaya hiyo ikiwemo ya maji itatekelezwa kama ilivyopangwa, waendelee kuwa na imani na Serikali yao.
BAADI ya wananchi wamkisiliza Majaliwa (Hayupo pichani)
Kuhusua suala la watumishi, alisema wilaya hiyo lazima iwe na watumishi wasafi wenye weledi wa kufanya kazi na lazima wahakikishe fedha za miradi zinazotolewa katika halmashauri hiyo zinalingana na thamani halisi ya mradi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel alisema atahakikisha watumishi wote wa umma waliohusika na wizi huo wanachukuliwa hatua stahili na kwamba tayari baadhi yao wameshafikishwa kwenye vyombo vya dola. 

No comments