Breaking News

VIJIJI VYOTE NCHINI KUPATIWA HUDUMA ZA MAJI SAFI:MAJALIWA.


MAJALIWA

Na Mwandishi Maalumu, Nachingwea.
WAZIRI Muu Kassim Majaliwa, amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote wakiwemo wa wilaya ya Nachingwea wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao, hivyo amewataka waendelee kuiamini.
Aliyasema hayo leo  Novemba 17, 2018 alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namatula ‘A’ na cha Mtua baada ya kuusimamisha msafara wa waziri mkuu huyo wakati akielea Kata ya Kilimarondo wilayani Nachingwea.

“Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini vikiwemo vijiji vya wilaya ya Nachingwea ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo.”
Waziri Mkuu Majaliwa, alisema serikali kupitia Kampeni ya Rais Dk. John Magufuli, ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.

Alisema, mbali na huduma ya maji, pia serikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

“Rais wetu Dk. John Magufuli, anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya ya Nachingwea. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.” Alisema.

Pia, alisema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Awali, Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, alimkabidhi Mwenyekiti wa kijiji cha Mpiluka saruji tani mbili na nusu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi Mpiluka.


No comments