Breaking News

MARAIS, DK, MAGUFULI NA KENYATTA WAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI (OSBP) * WAHIMIZA USHIRIKIANO NA UMOJA BAINA YA NCHI MBILI.


MARAIS, Dk. John Magufuli wa Tanzania (kushoto) na Uhuru Kenyatta wa Kenya, wakiwa wameshikana mkono wakati  wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya. (Picha zote na Ikulu)

            

                                     Na Mwandishi Wetu

MARAIS, Dk.  John  Magufuli wa Tanzania, na Uhuru Kenyatta wa Kenya, leo Desemba 01, 2018 wamezindua kituo cha huduma kwa pamoja mpakani (Ones Stop Border Post – OSBP) katika eneo la Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Taarifa ya Ikulu, kwa vyombo vya habari ilisema kuwa, pamoja na kuzindua ofisi za kituo hicho katika pande zote mbili, marais hao walipanda miti ya kumbukumbu na kukagua utoaji wa huduma zikiwemo za forodha na uhamiaji.

Kituo hicho ni miongoni mwa vituo 15 vya OSBP vinavyojengwa katika mipaka ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kurahisisha ufanyaji wa biashara miongoni mwa nchi hizo, kuharakisha huduma za mpakani, kuongeza mapato na kuimarisha usalama.

Ujenzi wa kituo cha Namanga OSBP umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali za Tanzania na Kenya.   Tanzania imegharimu shilingi Bilioni 22.365.

Tangu kianze kutoa huduma kituo hicho kimesaidia kupunguza muda unaotumiwa kukamilisha huduma za mpakani (clearance) kutoasaa 1 hadi dakika 15, na pia upandewa Tanzania ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka shilingi Bilioni 41 hadi kufikia shilingi Bilioni 58 zinazotarajiwa mwakahuu.

Wakizungumza baada ya kuzindua kituo hicho, Magufuli na Rais Kenyatta waliwashukuru wafadhili wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho (AfDBna JICA) na wametoa wito kwa Watanzania na Wakenya kuongeza biashara kupitia mpakahuo, huku wakitaka wafanyabiashara wadogo wasibughudhiwe.

“Kenya ni ya 3 kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa uwekezaji Tanzania kwahiyo Wafanyabiashara wa Kenya wanapopita hapa msiwaone kuwa ni maadui, halikadhalika Tanzania ni yenye mifugo mingi hasa ng’ombe kwahiyo Watanzania wanapopeleka nyama Kenya naowasikwamishwe” amesisitiza Magufuli.

“Sis itujione wana Afrika Mashariki, tuzilete nchi zetu pamoja na tuutumie umoja wetu wa watu takribani Milioni 200 kufanyabiashara na kunufaika, hapa mpakani sisi viongozi tupatumie kurahisisha biashara na nyie wananchi muwe huru kufanya kazi zenu ilimradi msivunje sheria nakufanya biashara haramu”amesema . Rais Kenyatta.

MARAIS, Dk. John Magufuli na Uhuru Kenyatta, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya leo.Aidha, Rais Magufuli ameahidi kushughulikia tatizo la maji katika eneo la Namanga kwa kuwapelekea maji yakutoka Longido ambako Serikali imejenga mradi mkubwa wa maji uliogharimu shilingi Bilioni 15.

Pia, Rais Magufuli ameishukuru AfDB baada ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki Gabriel Negatu kueleza kuwa imeridhia kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Malindi – Lungalunga – Tanga – Pangani – Bagamoyo inayounganisha Tanzania na Kenya, namradiwabarabarayaRumonge – Manyovu – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi inayounganisha Tanzania na Burundi.

Baada ya kuagana na Rais Kenyatta ambaye amerejea nchini kwake, Rais Magufuli akiwa njiani kwenda Arusha Mjini amekutana na wananchi wa Odonyosamba wilayani Arumeru na kuahidi kushughulikia tatizo la maji linalolikabili eneo hilo ambapo ameagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya mradi wa kusafisha maji kiasi cha shilingi Milioni 500 zitolewe wiki ijayo na pia amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.

Makame Mbarawa kufika katika eneo hilo ili kuangalia namna ya kufikisha maji ya kutoka mradi mkubwa wa maji Arusha Mjini kwa wananchi hao.

 Rais Magufuli pia amekutana na wananchi wa Mianzini katika Jiji la Arusha ambapo amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha Jiji la Arusha ikiwemo kujenga barabara za kisasa ndani ya Jiji hilo, kuwajali wafanyabiashara wadogo na kwamba kesho ataweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Arusha Mjini utakaogharimu shilingi Bilioni 520.

No comments