Breaking News

"OPARESHENI UVUVI HARAMU YAPAISHA MAPATO YA SEIKALI KUU".
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya        pamoja na baadhi washiriki wa operesheni              sangara  awamu ya III, Mwaka 2018 katika Kanda    ya Ziwa Victoria, jana.


                     Na Edward Kondela, Mwanza

OPARESHENI  za kudhibiti uvuvi haramu hapa nchini, zimeiwezesha Serikali Kuu,  kupata mrabaha wa Sh. Bilioni 2.2 kuanzia Desemba, 2017 hadi Novemba, 2018 kutoka Sh. Milioni 457.
Hayo yalibainishwa jana Desemba 01.12.2018 Jijini Mwanza na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, wakati akiongoza kikao cha kufanya tathmini ya operesheni sangara Kitaifa awamu ya tatu kwa mwaka 2018, kanda ya Ziwa Victoria. 
Kikao hicho kilihudhuriwa na maofisa waliohusika katika operesheni hiyo  ambapo alisema kiasi hicho cha fedha kimeongezeka kutokana na mafanikio ya udhibiti wa mianya ya utoroshaji fedha. 
“Mwaka 2017 mpaka tunafunga mwaka mwezi Desemba mrabaha wa Serikali Kuu kabla ya kufanya operesheni ulikuwa sh. Milioni 457, mwaka 2018 hadi mwezi Novemba mrabaha wa serikali kuu ni sh. Bilioni 2.290. 
OFISA Afisa Mfawidhi kanda ya Ziwa Victoria Didas     Mtambalike, akisoma tathmini ya kitaifa ya               operesheni hiyo.
“Kutoka sh. Milioni 457 mpaka sh. Bilioni 2.290 unaweza kuona kwamba ni ongezeko la zaidi ya asilimia 200, hii maana yake kulikuwa na utoroshaji mkubwa wa fedha ambazo zingeingia katika mfumo mkuu wa serikali,” alisema Ulega. 
Aidha, katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara wa samaki, Ulega alisema kabla ya kuanza kwa operesheni za kudhibiti uvuvi haramu, takwimu zilionyesha uwepo wa samaki wachanga zaidi ya asilimia tisini, lakini baada ya operesheni hizo samaki walianza kuongezeka kauli iliyoungwa mkono na wafanyabiashara hao ambao walisema samaki wakubwa wameanza kupatikana kwa wingi katika ukanda wa Ziwa Victoria.
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akitoa maelezo ya tathmini ya kitaifa ya operesheni sangara awamu ya III, mwaka 2018 kanda ya Ziwa Victoria kwa washiriki wa                 operesheni hiyo (hawapo pichani).


Awali, akiwasilisha taarifa ya operesheni sangara Kitaifa Awamu ya Tatu mwaka 2018 katika ukanda wa Ziwa Victoria, Ofisa Mfawidhi wa kanda hiyo  Didas Mtambalike, alisema tangu kuanza kwa operesheni hiyo Oktoba 18 mwaka 2018 hadi Desemba mosi mwaka 2018, sh. Bilioni 1.172 zilipatikana kutokana na malipo ya faini walizotozwa waliojihusisha na mtukio ya uvuvi haramu.
Mtambalike pia alisema zoezi hilo limewezesha vyombo vingi vya uvuvi na biashara za bidhaa za uvuvi kusajiliwa na kupatiwa leseni kutokana na elimu ambayo wavuvi walikuwa wakipatiwa ili kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.
“Kitu ambacho tumekibaini ni kwamba vyombo vingi sasa hivi vimesajiliwa vile vya uvuvi, vile ambavyo viko chini ya halmashauri vimesajiliwa lakini pia vile ambavyo viko chini ya Serikali Kuu vimesajiliwa ambavyo ni zaidi ya urefu wa mita 11,”alisema Mtambalike
Baadhi ya wadau wa uvuvi ambao walipata nafasi ya kutoa maoni yao kBAADHI wa washiriki wa kikao hicho wakimsikiliza Ulega (hayupo pichani).
Pia, pamoja na kulifanyia kazi ombi lao la kuendelea kuvua dagaa kwa kutumia taa zinazotumia mwanga wa jua kutokana na kusitishwa kwa ya taa hizo kwa shughuliza uvuvi hususana wa dagaa kutokana na uwepo wa madai ya samaki hao kuathiriwa na taa hizo, jambo ambalo  Ulega alisema serikali inalifanyia kazi.
Kikao cha tathmini ya operesheni sangara kitaifa awamu ya tatu mwaka 2018 katika kanda ya Ziwa Victoria kiliongozwa na Ulega na kufanya tathmini ya kutokomeza uvuvi haramu katika maeneo ya Singida, Sengerema, Ukerewe, Simiyu. 
Mikoa mingine ni Mwanza, Kagera, Geita na Mara ambayo yote yapo chini ya kanda ya Ziwa Victoria, ambapo kikao hivcho kimeridhishwa na mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika kudhibiti uvuvi haramu.

No comments